
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lembulung Lukumayi
maipacarusha20@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Dkt. Johannes Lembulung Lukumayi, amefanikisha matibabu ya kijana Japhet Mbayani, mkazi wa Nduruma, aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la figo na ambaye matibabu yake yaligharimu zaidi ya Sh milioni 10.
Dkt. Lukumayi aliingilia kati baada ya familia hiyo kushindwa kumudu gharama za matibabu, huku ikifikia hatua ya kupanga kuuza nyumba yao kwa Sh milioni 9 ili kupata fedha za kuokoa maisha ya mtoto wao.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa matibabu hayo katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha, familia ya Japhet ilimshukuru mbunge huyo kwa msaada mkubwa alioutoa, ikisema ameonesha moyo wa kujitolea na upendo kwa familia hiyo.
![]() |
| Kijana japheti aliyepatiwa msaada na mbunge Lukumay |
“Mbali na kutoa kiasi cha fedha, pia ametusaidia kutuunganisha na madaktari, lakini pia amekuwa akitupa moyo kuwa mgonjwa wetu atafanikiwa kupata matibabu Amesimama kama malaika ndani ya familia yetu,” alisema mmoja wa wanafamilia.
Familia hiyo ilieleza kuwa kabla ya kupata msaada wa mbunge huyo, walikuwa wamezunguka katika maeneo mbalimbali kutafuta msaada, lakini kutokana na gharama kubwa za matibabu walilazimika kuweka nia ya kuuza nyumba yao kwa Sh milioni 10
.
“ Tulikuwa tunauza nyumba kwa kiasi cha Sh milioni 10 ili tu kuokoa maisha ya kijana na mtoto wetu, lakini mbunge akaingilia kati na kusema atahakikisha kuwa anatusaidia katika hili,” alisema.
Kwa upande wao, wananchi wa Nduruma wamempongeza Dkt. Lukumayi kwa hatua hiyo, wakisema amedhihirisha uzalendo, upendo na kujali maisha ya wananchi anaowaongoza.
“Mbunge huyu amefanya jambo kubwa sana kwa kuwa ametusaidia. Nyumba ilikuwa inauzwa kwa ajili ya kupata Sh milioni 10 za matibabu. Tunapenda kuwashauri hata watu wengine kuhakikisha wanaiga mfano mzuri wa kiongozi huyu,” alisema mmoja wa wananchi.
Wananchi hao wameendelea kumshukuru Dkt. Lukumayi kwa kuendelea kuwa karibu na wananchi na kuingilia kati changamoto mbalimbali zinazowakabili, hususan katika masuala ya afya.
Mwisho

No comments:
Post a Comment