TAKUKURU TANGA YAENDESHA CHEMSHA BONGO ZUIA RUSHWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 9 August 2026

TAKUKURU TANGA YAENDESHA CHEMSHA BONGO ZUIA RUSHWA

 




Burhani Yakub,Tanga.


maipacarusha20@gmail.com 


Taasisi  ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Tanga imekuja na ubunifu wa aina yake kwa kuendesha Shindano la Chemsha Bongo zuia rushwa 2026,


Katika tamasha  hilo  shule ya msingi Ukombozi ilinyakua ubingwa baada ya kupata alama 96 dhidi ya ahule ya msingi  Bombo waliopata alama  91.


 Mashindano hayo yalikuwa na ushindani mkali hali iliyolazimu teknolojia ya VAR kutumika mara kwa mara kwa lengo la kundoa utata katika kumpata Msindi wa fainali za Shindano la Chemsha Bongo Zuia rushwa 2026, lililofanyika shule ya Sekondari Tanga Ufundi iliyopo Jijini Tanga.


Mgeni rasmi katika Tamasha hilo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga aliyewakilishwa na Afisa elimu wa Mkoa huo, Immanuel Kisango amesema atahakikisha shule zote zinakuwa na klabu za TAKUKURU.


Kisango ameeleze kuridhishwa kwake juu ya uelewa mpana ulioweza kidhihirisha na wanafunzi katika kujibu maswali yanayohusu mapambano dhidi ya rushwa akisema,wakiendelezwa kujengewa uwezo jamii kubwa itanusurika.


"Nina mshukuru Mkuu wa Mkoa kuniagiza kuja hapa,lakini pia nashukuru Katibu tawala kuridhia Mimi kumwakikisha mkuu wa mkoa,hapa nimejionea uwezo mkubwa waliopata watoto wetu,nitahamikisha shule zote zinakuwa na klabu za TAKUKURU"alisema Afisa elimu.


Ramadhani Ndwata ni Mkuu wa TAKUKURU mkoani Tanga,amesema  mchango wa wazazi unahitajika  katika kuwalea watoto wao kwenye maadili mema.


Ameelezea kuridhishwa kwake na ushirikiano uliooneshwa na wazazi katika malezi ya watoto hao kimaadili huku akisisitiza kuwa washindi watakaopatikana kupitia Chemsha Bongo zuia rushwa 2026 watakuwa mabalozi wa kuzuia rushwa kuanzia ngazi ya familia


Amesema, Chemsha Bongo hiyo ni mkakati wa muda mrefu wa TAKUKURU katika kujenga kizazi kinachochukia rushwa program aliyoieleza kuwa ni moja ya utekelezaji wa jukumu la kisheria.


Mkuu wa dawati la elimu kwa umma TAKUKURU Mkoani Tanga,Frank Mapunda amesema, kufanyika kwa mashindano hayo ni sehemu ya majukumu ya TAKUKURU yaliyoelelezwa katika kifungu cha saba cha sheria ya kuzia na kupambana na rushwa,sura ya 329 marejeo 2023.


Amesema,moja ya majukumu ambayo TAKUKURU inatakiwa kufanya ni kuhamasisha ushiriki wa umma katika masuala ya uzuiaji na mapambano dhidi ya rushwa.


Kufanyika kwa Tamasha hilo lililokuwa mashindano ya Chemsha Bongo zuia rushwa 2926 ni matokeo ya ubunifu uliioneshwa na TAKUKURU mkoa wa Tanga kwa kutumia mfumo wa kutengeneza mada mbalimbali juu ya rushwa.


Imeelezwa kuwa awali mashindano hayo yalikuwa na washiriki 32 ambao ni kutoka klabu wa wapinga rushwa wa tarafa nne zilizopo katika halmashauri ya Jiji la Tanga.


Katika Shindano hilo mshindi wa kwanza ameyakua zawadi ya kikombe kikubwa na Shilingi 200,000, wa pili kikombe kidogo na Shilingi 150,000, mshindi wa tatu ngao ya glasi na Shilingi 100,000 na mshindi wa nne amezawadiwa ngao ya plastiki na Shilingi 50,000.


        MWISHO 

.

No comments: