Dkt Samia awataka wakuu wa mikoa wakawe watumishi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 2 September 2026

Dkt Samia awataka wakuu wa mikoa wakawe watumishi

 



 

Mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com 


Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan, amewaambia wateuliwe wapya wa ukuu wa mkoa na katibu tawala kwamba hawajapeleka maeneo hayo, kuwa wafalme bali kuwa watumishi wa wananchi.


Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.


Amefafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba, Rais amekasimu madaraka yake katika eneo lililokatwa la mkoa na kukabidiwa wakuu wa mikoa.


“Wewe jichukulie kama rais wa eneo hilo, mkoa hauna fedha ni lako, umekumbwa na mazingira baada ya mvua kunyesha ni lako, kwa Rais ni msaada tu,” amesema na kuongeza kuwa;


“Unabeba dhamana ya mkoa, na unasema huu mkoa na watu wake ndio Taifa langu, hatuwapeleki pale mkale raha,” amesema Rais Dkt Samia.

No comments: