MLINZI ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA DEREVA AKITOKEA MSIKITINI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 9 September 2026

MLINZI ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA DEREVA AKITOKEA MSIKITINI

 


Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Andrew Kantimbo

Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com 


Hussein Idd Hussein (37), mlinzi wa Kampuni ya Ruge Security,mkazi wa Kayenzi Manispaa ya Morogoro, anashikiliwa na jeshi la polisi Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya Feisal Yaqoob Ally (43), dereva wa gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 680 EAY, mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Andrew Kantimbo alisema tukio hilo limetokea Septemba 9, 2026 majira ya saa 12 Alfajiri, katika eneo la kituo cha mafuta Puma kilichopo Mtaa wa Viwandani, Kata ya Kihonda, Manispaa ya Morogoro.


Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa akitoka jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza, alipofika katika eneo hilo na alisimama katika kituo hicho cha mafuta aliegesha gari lake kwa ajili kwenda kuswali katika msikiti uliopo karibu na kituo hicho.



Inadaiwa kuwa baada ya kutoka msikitini akielekea kwenye gari lake mtuhumiwa ambaye ni mlinzi alimtaka kumlipa kiasi cha shilingi 15,000 kwa kumlindia gari,lakini marehemu alikataa na kupanda kwenye gari kwa nia ya kuondoka ndipo

mlinzi alipofyatua risasi kwa kutumia bunduki na kumpiga dereva  na kichwani na kusababisha kifo chake hapo hapo.


Katika tukio lingine,jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watuhumiwa saba  kwa mauaji ya Zakaria Rashid Malika (57), Afisa Ardhi mkazi wa Kibao­ni Wilaya ya Kilombero.


Mauaji ya afisa huyo ardhi yaliyotokea Julai 19, 2026 katika Kijiji cha Kapolo CCM, Kata ya Kibaoni, Tarafa ya Ifakara, Wilaya ya Kilombero ambapo alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake na kumshambulia na kitu chenye makali na kumsababishia majeraha kwenye mwili wake na Ä·upelekea kifo.





Kamanda Kantimbo alisema julai 20,2026 polisi walitoa taarifa na kuwataka wananchi kutoa ushilikiano wa kuwasaka watuhumiwa ambapo kwa nyakati na maeneo tofauti walikamatwa watuhumiwa hao saba.


"Polisi baada ya kupokea taarifa kuhusu tukio hilo, lilifanya jitihada za kuwatafuta watuhumiwa hao kwa kushirikiana na wananchi na Watu saba walikamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuhusika katika mauaji hayo,"alisema. 


Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za awwli za upelelezi kukamilika.


Polisi linatoa wito kwa wamiliki wa Kampuni za ulinzi kuaji walinzi wenye weledi na wanaozjua sheria,taratibu na kanuni za matumizi sahihi ya silaha wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuzuia madhara kama haya kutokea.


Pia limewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola.


...

No comments: