MUME WA RAIS Samia Afariki Dunia leo Asubuhi, Mazishi yafanyika jioni hii - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 7 September 2026

MUME WA RAIS Samia Afariki Dunia leo Asubuhi, Mazishi yafanyika jioni hii




MUME wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Mwalimu Hafidh Ameir Hassan, amefariki dunia.

Taarifa za kifo cha Mwalimu Hafidh zilitangazwa leo asubuhi, Septemba 7, 2026, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratias Ndejembi, ambaye alieleza masikitiko makubwa kufuatia kuondokewa na kiongozi huyo wa familia ya Rais.





Kwa mujibu wa taarifa hiyo, marehemu alikuwa na umaiti wakati akipatiwa matibabu ya moyo katika Hospitali ya Mzena na mazishi yanatarajiwa kufanyika Kizimkazi, mkoa wa Kusini Unguja, ambapo ndugu, jamaa, viongozi wa serikali na wananchi wanatarajiwa kushiriki.

Marehemu Mwalimu Hafidh Ameir Hassan alikuwa mume wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na wameishi pamoja kwa miaka mingi, huku familia yao ikijaliwa watoto wanne.

Katika maisha yake ya umma, Mwalimu Hafidh alijulikana kwa maisha ya utulivu na kutokuwa mtu wa kujitokeza mara kwa mara katika shughuli za kisiasa na kijamii, licha ya mke wake kushika nyadhifa mbalimbali za juu serikalini hadi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa mbalimbali za wasifu wake zinaeleza kuwa alikuwa msomi na mtaalamu wa masuala ya kilimo, huku akitambuliwa pia kwa mchango wake katika malezi na maendeleo ya familia yake.

Kifo cha Mwalimu Hafidh, ambaye pia ni Baba wa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, kinakuja ikiwa Rais Samia anaendelea kulitumikia Taifa katika nafasi ya juu ya uongozi, hali inayowagusa Watanzania na wananchi wa Zanzibar kutokana na nafasi ya marehemu katika familia ya Rais na mchango wake Kwa nchi.

Makamu wa Rais, katika taarifa yake, alitoa salamu za pole kwa Rais Samia, familia ya marehemu na ndugu wote walioguswa na msiba huo.

Wananchi na viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuendelea kutoa salamu za rambirambi kwa Rais Samia na familia yake, huku mazishi yakifanyika leo alasiri Kizimkazi, mkoa wa Kusini Unguja

No comments: