Na Mwandishi Wetu
maipacarusha20@gmail.com
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limethibitisha kumkamata Godlisten Elisante Malisa akiwa na mwenzake usiku wa Agosti 31, 2026, kutokana na tuhuma za jinai zilizokuwa zikichunguzwa dhidi yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Malisa na mwenzake walifanyiwa mahojiano na Jeshi hilo kufuatia tuhuma hizo.
Polisi imesema baada ya mahojiano, Malisa na mwenzake wameachiwa kwa dhamana huku wakisubiri taratibu nyingine za kisheria kukamilishwa.
Taarifa hiyo ya Polisi imekuja baada ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kutoa wito kwa Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji kueleza mahali Malisa alipokuwa akishikiliwa na sababu za hatua hiyo.
![]() |
| Wakili Dickson Matata akiwa na Godlisten Malisa mara baada ya kuachiwa na Polisi |




No comments:
Post a Comment