RC MSTAAFU GEITA GABRIEL ROBERT AIPONGEZA VETA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 30 September 2026

RC MSTAAFU GEITA GABRIEL ROBERT AIPONGEZA VETA



MKUU wa Mkoa mstaafu wa Geita, mhandisi Gabriel Robert mwenye kofia akipewa maelezo na uongozi wa veta


Mwandishi wetu, Geita 


maipacarusha20@gmail.com


MKUU wa Mkoa mstaafu wa Geita, mhandisi Gabriel Robert ameipongeza Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kwa namna inavyowapa ujuzi vijana mbalimbali ikiwemo kwenye sekta ya teknolojia ya madini.

Mhandisi Gabriel ameeleza hayo alipotembelea banda la VETA lililopo kwenye maonyesho ya tisa ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika viwanja vya Dkt Samia Suluhu Hassan manispaa ya Geita.

Mhandisi Gabriel amejionea shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye banda la VETA na kuwaasa vijana wafike eneo hilo kwani kuna manufaa makubwa kwao.

Amesema mapinduzi yanayofanywa na Serikali ni makubwa kupita taasisi zao hivyo vijana wanapaswa kujiunga kwa wingi VETA ili wapate ujuzi.

"Ndoto na dhamira kubwa imebaki kwenye teknolojia ya madini nimeona VETA walivyo mabingwa wanachukua vijana ambao wanapata ujuzi wanajifunza VETA ili kujiajiri na kuajiriwa," amesema mhandisi Gabriel.

Amesema vijana wengi hivi sasa wanajishughulisha na uchimbaji wa madini kwa hiyo wakipitia VETA wanakuwa wanatambulika kitaalamu kuliko kufanya jambo bila kusomea.

"Watu waliopitia VETA wananufaika kupitia ujuzi walioupata kwani wameandaliwa kupigana vita vya kiuchumi kupitia unyago wa teknolojia walioupata VETA," amesema mhandisi Gabriel.

"Wito wangu kwa watu wa ndani ya Tanzania wasidharau VETA, waende wakasome wapate ujuzi wasiseme watapiga ramli, dunia ya sasa imebadilika kupitia teknolojia mbalimbali," amesema mhandisi Gabriel.

Amesema watu waliopitia VETA wana ujuzi mkubwa na kila teknolojia iliyopo na inayopatikana kupitia vyuo vyao wanapata ujuzi mkubwa kwa kuweza kujiajiri au kuajiriwa.

"Ushauri wangu kwa VETA waendelee kufanya utafiti kwa elimu ya leo ili vijana waendeleee kupata unyago wa teknolojia na kuzidi kunufaika kupitia VETA," amesema mhandisi Gabriel.


MWISHO

No comments: