WATANO WAFARIKI KATIKA AJALI YA KIFUSI MGODINI KITATA, GAIRO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 7 September 2026

WATANO WAFARIKI KATIKA AJALI YA KIFUSI MGODINI KITATA, GAIRO

 


Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Japhar Kubecha

Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com 


Watu watano wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi katika duara la uchimbaji wa madini kwenye mgodi wa Kitaita, wilayani Gairo, mkoani Morogoro.


Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Japhar Kubecha, zimeeleza kuwa watu tisa waliingia katika duara hilo kinyemela majira ya usiku kwa ajili ya shughuli za uchimbaji wa madini.


Kubecha amesema watu hao, ambao hutambulika kwa jina la “wadudu,” walipatwa na ajali hiyo baada ya kifusi kuwaangukia wakiwa ndani ya duara hilo.


Amesema miili ya watu watano imepatikana, huku mwili mmoja tayari ukitambuliwa kuwa ni wa mkazi wa Kilindi.


Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, taarifa za awali zinaonyesha kuwa baadhi ya marehemu wanatoka nje ya Wilaya ya Gairo.

No comments: