Kamati Tendaji ya IPU Yakutana Arusha Kuelekea Mkutano wa 153 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 3 October 2026

Kamati Tendaji ya IPU Yakutana Arusha Kuelekea Mkutano wa 153

 




Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 3 Oktoba 2026, ameongoza kikao cha Kamati Tendaji ya IPU kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).


Kikao hicho ambacho pia kimehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ni sehemu ya maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Arusha, Tanzania, Oktoba 5-9, 2026.


Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na unatarajiwa kuhudhuriwa na takribani washiriki 2,000 kutoka mabunge 183 wanachama wa IPU, wakiwemo Maspika, Wabunge, Makatibu wa Mabunge na maafisa mbalimbali kutoka mabunge duniani.

No comments: