MILTON DICK WA AUSTRALIA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA IPU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 9 October 2026

MILTON DICK WA AUSTRALIA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA IPU

 




mwandishi wetu, maipac


maipacarusha20@gmail.com


SPIKA wa Bunge la Australia, Milton Dick, amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) baada ya kupata kura 182 sawa na asilimia 56 ya kura zote 

Akitangaza matokeo ya washindi, Rais anayemaliza muda wake Dkt Tulia Ackson amesema nafasi ya pili ilichukuliwa na Spika wa Azbeijan  Ms.Sahiba Gafarova  aliyepata kura 124 sawa na asilimia 38 na mgombea wa mwisho ni Spika wa Bunge la Chile Rojo Edward Silver aliyepata kura 21 sawa na asilimia 6.


Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Milton Dick, ameahidi kuimarisha demokrasia, amani na ushirikiano wa kimataifa, akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa umoja huo kwa kumwamini na kumpa dhamana ya kuongoza taasisi hiyo.


Amesema anapokea jukumu hilo kwa unyenyekevu na kutambua wajibu mkubwa aliopewa wa kuhakikisha kila taifa, bila kujali ukubwa wake, utajiri au ushawishi wake, linaheshimiwa na kupata nafasi ya kusikilizwa katika jukwaa la kimataifa.


"kuchaguliwa kwangu ni ukumbusho kwamba demokrasia, kuheshimiana na ushirikiano bado ni misingi muhimu katika kuunganisha mataifa na kutafuta majibu ya changamoto zinazolikabili dunia," amesema

No comments: