MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE AJINYONGA MOROGORO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 5 October 2026

MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE AJINYONGA MOROGORO


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Andrew Kantimbo


Na Lilian Kasenene ,Morogoro 


Maipacarusha20@gmail.com 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linachunguza tukio la kifo cha mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 11, anayesoma katika Shule ya Msingi Mwenge, Kata ya Kingolwira, Wilaya ya Morogoro, ambaye inadaiwa amefariki kwa kujinyonga.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Andrew Kantimbo, tukio hilo limetokea Oktoba 2, 2026, saa 1:00 usiku.


 Amesema mwanafunzi huyo alidaiwa kujinyonga kwa kutumia mkanda wa begi aliokuwa ameufunga dirishani kwa madai ya kutaka kujiua.


Taarifa hiyo inaeleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini kwa kina mazingira na sababu zilizopelekea mwanafunzi huyo kuchukua hatua hiyo.


Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


Kamanda Kantimbo amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.

........

No comments: