Rais Samia Suluhu Hassan, ameyahimiza mabunge duniani kushirikiana, kujenga imani ya wananchi na kusimamia matumizi ya rasilimali za umma huku yakishirikiana kukabiliana na changamoto za dunia.
Dkt Samia, ameyasema hayo leo, Oktoba 5, 2026 katika ujumbe wake kwa washiriki wa mkutano wa IPU unaofanyika Arusha kuanzia Oktoba 5 hadi 7, mwaka huu.
Amesema dunia inashuhudia ongezeko la sintofahamu za kijiografia na kisiasa, migogoro ya muda mrefu pamoja na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazokwamisha jitihada za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mkuu huyo wa nchi, amesema changamoto nyingi zinazozikabili nchi kwa sasa haziwezi kutatuliwa na Taifa moja pekee, bali zinahitaji ushirikiano wa kimataifa unaoshirikisha Serikali na mabunge.

No comments:
Post a Comment