MAKAMU WA RAIS ATAKA KUFUFULIWA KILIMO CHA MAUA ARUSHA, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi naye afuraishwa na ujio wa mashamba hayo ya maua - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 10 November 2026

MAKAMU WA RAIS ATAKA KUFUFULIWA KILIMO CHA MAUA ARUSHA, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi naye afuraishwa na ujio wa mashamba hayo ya maua





Na Mwandishi wetu,Arusha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, amesema thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya bustani nchini imekaribia kuongezeka maradufu ndani ya miaka minne, ikifikia dola za Marekani milioni 569 mwaka 2024, huku Serikali ikiendeleza taratibu za kufungua masoko mapya katika nchi 14.

Ndejembi amesema hayo leo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa na Mazao ya Bustani, HortiLogistica Africa 2026, katika viwanja vya TGT, Halmashauri ya Arumeru - Arusha.

Amesema mauzo hayo yameongezeka kutoka dola milioni 290.7 mwaka 2020, huku tasnia hiyo ikikua kwa wastani wa asilimia tisa hadi 12 kwa mwaka.

Amesema taratibu za kufungua masoko mapya zitaendelezwa mwaka wa fedha 2026/2027, sambamba na kuwajengea uwezo wakulima kukidhi viwango vya kimataifa. Akitembelea mabanda kabla ya ufunguzi, ameielekeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kubaini bidhaa zinazohitajika katika masoko hayo na viwango vyake vya ubora ili kuwaongoza wazalishaji.

Amesema uzalishaji wa mazao ya bustani umeongezeka kutoka tani milioni 8.44 mwaka 2022/2023 hadi tani milioni 9.78 mwaka 2024/2025, sawa na ongezeko la asilimia 15.9. Kwa upande wa parachichi, uzalishaji umefikia tani 203,473 mwaka 2025/2026, kutoka tani 149,340 mwaka 2020/2021, huku kiasi kinachouzwa nje kikifikia tani 52,593.72 zenye thamani ya Sh bilioni 255.4.

Kutokana na fursa hizo, Ndejembi ameielekeza Wizara ya Kilimo kuimarisha uzalishaji wa miche bora, uhifadhi wa mazao na utoaji wa mafunzo ili kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika kilimo cha parachichi.

Aidha, ameitaka wizara hiyo kufufua kilimo cha maua kwa kutumia mashamba yaliyopo Arusha yenye miundombinu ya uzalishaji.




Amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza mapato ya fedha za kigeni, akikumbusha kuwa maua yaliyozalishwa Arusha hapo awali yalikuwa na soko kubwa duniani.

Amepongeza mchango wa wakulima na wajasiriamali, hasa walio chini ya TAHA wana nafasi kubwa sana ya kukuza mitaji yao lakini hata masoko ya nje ya nchi


Aliitaka TAHA kuendelea kusimamia lakini kubuni mbinu nyingi ambazo zitaweza kuwasaidia wakulima kufanya kilimo cha kisasa zaidi.


Naye mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Dkt Johannes Lukumayi alisema kuwa Agizo la makamu wa raisi juu ya urudishaji wa mashamba ya maua ni faraja kubwa sana kwa wananchi


Dkt Lukumayi alisema kuwa mashamba hayo yalikuwa na uwezo wa kuzakisha ajira za kudumu nyingi sana na hata mashamba hayo ya maua yalipositisha uzalishaji wake zipo baadhi ya familia ambazo ziliteseka kwa kukosa ajira


"Hili suala la mashamba ya maua ambalo limezungumzwa hapa Leo nilishashawai kuuliza na kufuatilia suala hili nashukuru kwa kuwa jamii yangu sasa imepata majibu mazuri"aliongeza Dkt Lukumayi


Wakati huo huo alisema kuwa yeye kama mbunge wa Jimbo Hilo Bado anaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanabuni miradi ambayo itakuwa na tija kwa jamii


Mwisho

No comments: