MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MKE WA KATIBU WA MAREMA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 11 November 2026

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MKE WA KATIBU WA MAREMA

 



Na mwandishi wetu, Mirerani 


MAMIA ya wakazi wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wamejitokeza kwa wingi kwenye mazishi ya marehemu Laura Lawrence Massawe ambaye ni mke wa Katibu wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Tariq James Kibwe.


Afisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini wa Mirerani, (RMO) George Kaseza, ameongoza mamia hao katika mazishi yaliyofanyika Mirerani na maziko eneo la Kia Mkoani Kilimanjaro.


Akizungumza kwenye mazishi hayo RMO George Kaseza ametoa pole kwa Kibwe na familia yote kwa ujumla kutokana na msiba huo.


Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji madini Tanzania (FEMATA) Peter Kabepera akizungumza kwa niaba ya Rais wa FEMATA John Bima ametoa pole na rambirambi kwa msiba huo.


"Rais Bina yupo nje ya nchi hivyo hakuweza kufika msibani ila amenituma nimwakilishe katika msiba huu mzito wa kiongozi wetu kuondokewa na mwenza wake," amesema Kabepera.


Mwenyekiti wa MAREMA Elisha Nelson Mnyawi amewapa pole wafiwa na kuwapa faraja kutokana na msiba huo uliowapata.


"Nawapeni moyo na usiharibu kesho yako kwani Mungu ni mwema unapokwenda ni kuzuri zaidi kuliko ulipotoka," amesema Elisha.


Mwenyekiti mstaafu wa MAREMA, Justin Nyari ametoa pole kwa Kibwe na familia yote ya marehemu kwa msiba huo uliowapata.


Diwani wa kata ya Mirerani Salome Nelson Mnyawi amewaasa watoto wa marehemu waendelee kumpenda baba yao katika muda wa maisha yao.


"Kibwe, Mungu akubariki usimame kama baba ili watoto wasipate upweke nanyi watoto muheshimuni baba yenu ndiyo sababu Mungu hakuwachukua wote wawili," amesema Salome.


MWISHO

No comments: