![]() |
| Rais Samia Suluhu Hassan |
![]() |
| Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wakati akirekodi kipindi cha Royal Tour |
| Mnyama Twiga moja ya kivutio kikubwa cha watalii |
Mwaka Mmoja wa Rais Samia Suluhu sekta ya Utalii.
Mapato yaongezeka,mamia ya watalii watua nchini,Tuzo 14 za kimataifa. Mussa Juma,MAIPAC Sekta ya Utalii bado inaongoza kwa kuchangia fedha nyingi za kigeni katika pato la Taifa. Mchango wa sekta hii wa fedha za kigeni ni asilimia 25 na katika pato la taifa kwa ujumla sekta hii inachangia zaidi ya asilimia 17.5 huku ikitoa ajira takriban watu1.6 milioni. Hivyo sekta hii ni nyeti sana kwa mustakabari wa Taifa,hata hivyo kati ya mwaka 2019/20 sekta hii iliathirika sana na ugonjwa ya uviko -19. Kuathirika kwa sekta hii, kulitokana na maelfu ya watalii kusitisha safari zao, lakini pia mashirika makubwa ya ndege yalisitisha safari. Athari za janga la ugonjwa wa UVIKO-19 katika sekta ya Utalii kulisababisha kupotea kwa zaidi ya dola 4 trilioni kwa uchumi wa dunia kwa mujibu wa ripoti ya shirika la biashara na maendeleo la umoja wa Mataifa(UNCTAD) na shirika la umoja wa mataifa la Utalii(UNWTO). Ripoti hiyo inaeleza anguko kubwa la kuwasili kwa watalii duniani kote mwaka 2020 kulisababisha hasara ya dola 2.4 trilioni. Katika nchi zinazoendelea watalii wa kimataifa walipugua kwa karibu bilioni 1 au asilimia 73 mwaka 2020 na katika robo ya kwanza ya mwaka huu 2021 kushuka kwa watalii ni karibu asilimia 88 ilieleza ripoti hiyo ya umoja wa mataifa. Hapa nchini mwaka 2020, Wizara ilitarajia yamaliasilina Utalii ilipanga kupokea watalii 1,867,000. Makisio hayo yalikuwa ni kabla ya kutokea kwa janga la UVIKO-19 na baada ya mlipuko Wizara ilifanya tathmini ya athari za ugonjwa huo katika sekta ya utalii na kuweka makisio mapya ya jumla ya watalii 437,00.
Mwaka mmoja wa Rais Samia alivyofufua Sekta ya Utalii. Tangu kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya Sita, Rais Samia Suluhu amefufua sekta ya Utalii nchini,kutokaa na jitihada zake binafsi za kutangaza utalii, kutokana na ziara ya Royol Tour lakini pia kuridhia itifaki za shirika la afya Duniani katika kupambana na ugonjwa wa Uviko-19. Nchi imefanya vizuri zaidi katika kipindi cha uviko- 19 na kupewa tuzo na taasisi umoja wa mataifa nchini hispania.
Waziri wa maliasili na utalii, Dk Damas Ndumbaro anasema mwaka mmoja wa Rais Suluhu Hassan idadi ya watalii imeongezeka mwaka 2020kuliku wanawatalii 620,000 lakini takwimu 2021 watalii wa nje 900,022 na watalii wa ndani 700,088 Dk Ndumbaro anasema katika kipindi cha uviko takriban , watali milioni 1.7 walitembelea vivutio vyautalii.
Anasema katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu, katika Kipindi cha uviko- 19, Taifa limevunja rekodi ya watalii wa ndani. Alisema ongezeko la watalii katika mwaka mmoja wa Rais Samia ni asilimia 40.2 kutoka mwaka 2020 hadi 2021 ya watalii waliotembelea hifadhi. Mapato 2020 mapaato watalii yapaa. Waziri Ndumbaro anasema mwaka mmoja wa Rais Samia Suluu mapato ya Utalii yameongezeka sana. Anasema mwaka 2020 watalii wa ndani waliingiza kiasi cha sh 9 bilioni lakini 2021 watalii wa ndani wameingia kiasi cha sh 12.4 bilioni. Waziri anasema watalii wa nje mwaka 2020waliingiza Dola milioni 715 lakini 2021, watalii wa nje wameingiza dola bilioni 1.24 .
Anasema mwaka mmoja wa Rais Samia, Tanzania imeweza kupata tuzo 14 za kimataifa za masuala ya Utalii na uhifadhi. Anasema Tanzania ilifanikiwa kuwa mwenyeji wa kwanza kwa maonesho ya utalii wa afrika ya Mashariki mwezi octoba jijini Arusha.
Mafanikio ya Royal Tour
Waziri anasema kumekuwepo na Mafanikio makubwa katika kazi ya kutangaza Utalii ya Royol Tour ambapo Rais Samia Mwenyewe aliongoza kutengenezwa filamu ya vivutio vya utalii. Anasema kutokana na Royol Tour Makampuni 30 ya mawakala wa Utalii kutoka nchi za Marekani na ulaya wametembelea nchini na kuanza kuleta watalii. Samia anasema Kampuni ya Utalii kutoka Bulgaria baada ya kuvutiwa na Royol Tour imepanga kuja nchini kujenga hoteli za nyota tano, tano katika hifadhitano za taifa. Anasema mwaka mmoja wa Rais Samia, wameongeza juhudi za kutangaza utalii, kuzindua mazao mapya ikiwep Utalii fukwe, Utalii wa meli, utalii michezo, ikiwepo Yanga kuvaa jezi lenye logo ya Visit kilimanjaro na Zanzibar Simba visit Tanzania. “tumezindua Utalii Golf Arusha tumeimarisha uhifadhi, Jeshi Usu, limeimarishwa pia”anasema Anasema Mwaka mmoja wa RaisSamia, Ushirikiano na sekta binafsi umeongezeka, vikao zaidi 20 vya sekta vimefanyika.
TANAPA waeleza mafanikio mwakammoja wa Rais Samia. Kamishna wa uhifadhi wa Shirika la hifadhi za Taifa, William Mwakilema anasema mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu, TANAPA imepata mafanikio makubwa. Mwakilima anasema mwaka mmoja wa Rais Samia Mapato yameongezeka kutoka sh 86.2 bilioni mwaka 2020 hadi kufikia sh 127.9 bilioni. Amesema mwaka mmoja wa Rais Samia Utalii umeimarika sana nchini, ikiwepo katika jiji la Arusha kwani kazi nzuri imefanyika. Anasema TANAPA ambayo inasimamia eneo la asilimia 11.6 la nchi nzima ambalo kuna vyanzo vingi vya maji na maeneo yaliyohifadhiwa , usimamizi umeimarika sana . “hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeendelea kupata tzo kuwa hifadhi bora lakini pia imepata tuzo ya utoaji huduma bora za viwango mwaka 2021”anasema Mwakilema anasema kutokana na fedha za uviko-19, miundombinu ya hifadhi nyingi inaendelea kukarabatiwa lakini pia uhifadhi na utalii kuimarishwa. Kamishna wa uhifadhi wa Ngorongoro, Dk Fredy Manongi pia anasema mwaka mmoja wa Rais Samia mapato yameongezeka kutoka sh 31 bilioni mwaa 2020 hadi kufikia sh 102 bilioni mwaka 2021.
Anasema Rais Samia pia katika mwaka wake mmoja, ameweza kutoa kiasi cha sh 6 Bilioni kukarabati na miundombinu ya hifadhi. Katibu Mtendaji wa chama cha mawakala wa Utalii(TATO) Sirili Akko anasema Mwaka mmoja wa Rais Samia sekta ya Utalii imeimarika sana. “kitendo cha mama kushiriki moja kwa moja kupitia Royol Tour kutangaza Utalii kumevutia watalii wengi duniani hata kabla ya filamu kuanza kurushwa yote rasmi”anasema Anasema pia ushirikiano baina ya wizara ya Maliasili na Utalii na wadau umeongezeka na hivyo kupunguza changamoto. Mwenyekiti wa chama cha waongoza Watalii,(TTGA) Emmanuel Mollel pia anaeleza mwaka mmoja wa Rais Samia umekuwa na mafanikio makubwa. “tumeona waongoza utalii kwa mara ya kwanza wamekusanywa na serikali na kupewa mafunzo lakini mazingira ya kazi yanaendelea kuboreshwa”anasema Huu ndio mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu ambao umekuwa na faraja katika sekta ya Utalii chini. Mussa Juma ni Mkurugenzi wa MAIPAC |




No comments:
Post a Comment