MABADILIKO YA TABIA NCHI YAUA MIFUGO ZAIDI YA 92,000 WILAYANI SIMANJIRO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 29 March 2022

MABADILIKO YA TABIA NCHI YAUA MIFUGO ZAIDI YA 92,000 WILAYANI SIMANJIRO

Afisa Kilimo na Mifugo, Dk Swaleeh Masaza kulia akitoa takwimu za mifugo liyokufa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi wilayani Simanjiro


Baadhi ya wanahabari wakisikiliza wasilisho la utafiti huo

wanahabari wakichukua taarifa za kina juu ya utafiti huo

Afisa mabadiliko ya tabia nchi toka PINGOs Forum Gedion Sanago akijibu maswali toka kwa wanahabari baada ya wasilisho la tafiti juu ya uwezo wa elimu ya asili kukabiliana na majanga

 NA: MAIPAC, ARUSHA

Jumla ya mifugo 92,047imekufa wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara,kutokana na  mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamesababisha ukame na kukauka vyanzo vya maji katika wilaya hiyo.

Afisa Kilimo na Mifugo,Dk Swaleeh Masaza akizungumza leo Machi 28,2022,katika uzinduzi wa utafiti juu ya uwezo wa jamii za  kifugaji kukabiliana na majanga,alisema kati ya mifugo Ng'ombe waliofariki ni  46,028.

Amesema Kondoo 21,046 walifariki,Mbuzi 21,070 na Punda 2003 hata hivyo,elimu ya asili iliyopo katika jamii hizo imesaidia sana kupunguza athari zaidi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mtafiti wa masuala ya mazingira Enock Changula amesema katika utafiti uliofanywa katika vijiji vitano wilaya ya Simanjiro umebaini elimu ya asili imesaidia sana jamii ya kifugaji kukabiliana na majanga.

Amesema elimu hiyo imesaidia jamii kukabiliana pia na magonjwa, Mafuriko lakini pia upatikanaji wa habari na kupashana habari.

"Mfumo wa wafugaji kuhamahama umeonekana kuwa na faida katika utunzwaji wa mazingira lakini pia unawezesha boresha ardhi ambayo imekuwa kivutio cha wanyamapori pia "Amesema

Afisa mabadiliko ya tabia nchi  na mazingira wa shirika la PINGOS Forums Gidion Sanago amesema utafiti huo umebainisha umuhimu wa kutambulika,kulindwa na kuendelezwa elimu ya asili katika kukabiliana na majanga.

"Tunawaomba watungaji wa sera waanze kuthamini,kutambua na kuingiza  elimu hiyo katika utungaji  sera za nchi "amesema.

Afisa wa jinsia na maendeleo ya jamii wa PINGOS Forums,Nailejileji Tipap amesema wahanga wakubwa wa mabadiliko ya tabia nchi ni wanawake na watoto.

"Elimu ya asili imeweza kutumika katika kukabiliana na majanga hata magonjwa ya akina mama na watoto"amesema.

No comments: