WASAKWA KWA MAUAJI YA SIMBA WATATU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 29 March 2022

WASAKWA KWA MAUAJI YA SIMBA WATATU



SIMBA hao waliouwawa maeneo ya mswakini Babati
 

Mwandishi wetu 

  Kikosi maalum cha Askari  wa Mamlaka ya usimamizi wanyamapori (TAWA) Kanda ya Kaskazini kimeanza msako katika vijiji vinavyozunguka eneo la mapito ya wanyamapori la Mswakini lililopo mpakani mwa mkoa wa Manyara na Arusha kubaini waliohusika na kuuwa simba watatu.
Kaimu Kamanda wa Uhifadhi wa TAWA, Kanda ya Kaskazini Peter  Mbanjoko leo Machi 29,2022 amesema Simba hao wameuawa juzi katika eneo hilo na wamechukuwa baadhi ya viungo.

"Tumepata taarifa za kuuawa Simba hao na askari wapo eneo la tukio kuwasaka waliohusika na mauaji hayo kwani ni kinyume cha sheria"amesema

Amesema kuna taarifa za watu kujeruhiwa na simba hao kabla ya kuwaua ambao watu hao wamejificha na wanatafutwa.

"Hakuna sababu yoyote ya kuuwa Simba huu ni ujangili na tunawasaka watuhumiwa na walipatikana watafikishwa kwenye vyombo vya sheria"alisema

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye anahifadhiwa jina akizungumza amesema Simba hao waliuliwa na vijana wa jamii ya kifugaji baada ya simba kula Mifugo.

"Hawa simba walikuwa wakisakwa na vijana wa kifugaji baada ya kula Mifugo na baada ya kuwaua wamekimbia"amesema

Katika eneo la Mapito ya Wanyamapori la Mswakini na kwa kuchinja  lilipo kati kati mwa hifadhi za Taifa za Tarangire na Manyara kuna idadi kubwa ya mifugo kutoka wilaya za jirani mkoani Manyara ambao hufuata madini chumvi  katika eneo la Ziwa Burunge na ziwa Manyara.

Mkuu wa wilaya ya Babati mkoa Manyara, Lazaro Twange akizungumzia matukio ya ujangili katika maeneo ya Mapito ya wanyama ameonya kuchukuliwa hatua kali watakaokamatwa.

"Tanatoa elimu umuhimu wa uhifadhi na kupiga vita ujangili sasa wale ambao wanaendelea kuvamia maeneo ya hifadhi vja kufanya ujangili hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa"amesema.


No comments: