WANAWAKE WA JAMII YA KIFUGAJI WA KIBARBEIGI WAPEWA MILIONI 16 KUKOPESHANA WAO KWA WAO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 29 March 2022

WANAWAKE WA JAMII YA KIFUGAJI WA KIBARBEIGI WAPEWA MILIONI 16 KUKOPESHANA WAO KWA WAO

Wamama wa kifugaji wakifurahia ruzuku walizopatiwa na taasisi ya chemchem Association 
 


Walter Pallangyo meneja wa chemchem association akitoa fedha za ruzuku kwa wanawake wa jamii ya kifugaji wa barbeigi  katika eneo la burunge WMA wilayani Babati 
 

NA: MAIPAC ,Babati

 Wanawake, wakiwepo wa jamii ya Kibarbeig katika eneo la hifadhi ya Jamii ya  wanyamapori ya Burunge wamepewa  ruzuku na Taasisi ya Chemchem association kiasi cha sh 16 milioni ili kukopeshana.

 Meneja wa Chemchem Association  ambayo ni taasisi iliyopo chini ya mwekezaji wa shughuli za Utalii ya Chemchem,Walter Pallangyo amesema lengo la kutoa ruzuku hiyo,ni kuongeza uwezo wa vikundi kukopeshana na kutambua mchango wa wanawake katika uhifadhi.

Pallangyo alikabidhi milioni ,7 kwa vikundi saba, ikiwa ni awamu ya pili baada ya kupewa million tisa.

Alisema Chemchem kama wawekezaji katika eneo hilo, ambao wanafanya utalii wa picha na hoteli za kitalii, wanataka wanawake katika eneo hilo, kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa uhifadhi, kupiga vita ujangili na kunufaika na utalii.

Walter alisema kutokana na faida za uhifadhi chemchem katika eneo hilo tayari imetoa bus ya usafiri wa wanafunzi, imejenga madarasa,imekarabati nyumba za walimu na vyoo,  imejenga vituo vya afya na kununua madawati kwa shule zilizopo katika eneo hilo la hifadhi ya jamii.


Afisa Mtendaji wa kijiji cha vilima vitatu,wilayani Babati, Seleman Juma alisema kutolewa na fedha hiyo faida ya kutunza mazingira, kupiga vita ujangili .

Aliwataka wanawake hao kutumia fedha hizo kama ilivyokusudiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa vikundi vilivyonufaika,  Flora Godson alishukuru Chemchem kwa msaada huo na kueleza watatumia fedha kama ilivyokususudiwa kukopeshana wao kwa wao

Alisema fedha hizo zitaongeza mikopo yao na hivyo kupanua biashara zao.

No comments: