Mauwaji ya Twiga kwa ajili ya biashara haramu ya nyama na viungo yaibuka ,.Mmoja afungwa miaka 20, wafadhili wasakwa - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 22 June 2022

Mauwaji ya Twiga kwa ajili ya biashara haramu ya nyama na viungo yaibuka ,.Mmoja afungwa miaka 20, wafadhili wasakwa



MAIPAC TEAM -Babati

Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache barani Afrika, ambayo yameweza kudhibiti matukio ya ujangili wa wanyamapori hasa Tembo.

Matukio ya ujangili  Tembo na Faru yalikuwa yameshamiri  miaka ya nyuma lakini kuanzia mwaka 2006, yalidhibitiwa na kusababisha kuongezeka kwa Tembo na Faru kwa kiasi kikubwa.

Hata hvyo, baada ya kudhibitiwa ujangili wa Tembo na Faru, sasa kumeibuka  ujangili wa kuuwa wanyama kwa ajili ya biashara yaharamu ya nyama  na baadhi ya viungo.

Biashara hii  haramu, imeibuka katika maeneo ya mapito ya wanyama(shoroba) ya kwakuchinja na Mswakini, katika mikoaya Arusha na Manyara, kaskazini mwa Tanzania.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, kupitia mradi infoNile kupambana na ujangili katika nchi za Afrika ya Mashariki, umebaini ujangili huu mpya unafanywa kwa ushirikiano baina ya wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya mapito yawanyama na wageni kutoka nje yavijiji.

Jeremiah Peter ni mkazi wa kijijicha vilima vitatu, wilayani Babati anaeleza kuwa, tangu kuanza kuibuka matukio ya Twiga kuuawa mwezi Januari imebainika kuna kikundi ambacho kinafanya matukio hayo.

“kuna baadhi ya wananchi ambao ni wenyejiwa vijiji vyetu wanashirikiana na watu kutoka nje ya vijiji kufanya uhalifu huu”anasema

Afisa wanyamapori wa wilaya ya Babati Christopha Laizer anasema tangu kuibuka matukio haya tayari watuhumiwa zaidi ya watano  wamekamatwa na baadhi wakiwa na nyama .

Laizer anasema tayari kuna kesi mbili mahakamani na watu waliokamatwa wakituhumiwa kuhusika na ujangili wa Twiga .

“tuna Kesi ya mtuhumiwa Mashaka  wa kijiji chavilima vitatu na tuna shauri jingine la watuhumiwa watatu, ambaoniAmos  Makala, Twaha Idd na Jackson Mwenda”alisema

Laizer anasema upelelezi wa matukio haya unaendelea na lengo ni kubaini wanaofadhili uwindaji huu haramu na biashara hii haramu ya nyamapori na viungo na mafuta.

“tumebaini biashara ya nyama ilikuwa inafanyikakatika mji wa magugu lakini tumedhibiti baada ya kukamata watuhumiwa lakini, bado tunasaka wafadhili wake”alisema

Anasema hivi sasa wameimarisha  ulinzi kwa kushirikiana baina ya askari  wa jumuiya  ya jamii ya  wanyamapori ya Burunge( burunge WMA) , Askari  halmashauri, Askari wa mamlaka ya usimamizi wanyamapori(TAWA) , askari wa taasisiya wawekezaji ya chemchem na askari wa hifadhi ya Taifa yaTarangire.

“tunaendelea  vizuri na operesheni zetu kuhakikisha tunakomesha aina hiiya ujangili”alisema

 

Mmoja afungwa miaka 20kwa kupatikana na nyamaya twiga

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa waManyara, june 9, 2022, imemuhukumu kifungo cha miaka 20,  Mashaka Boay(41) mkazi  wa kijiji chavilimavitatu, baada ya kupatikana na nyama ya twiga yenye thamani ya sh 34 milioni.

Hakimu mkazi Kimario Said  alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa na nyama hizo march 23 mwaka huu ikiwa ni kinyume cha sheria.

Licha ya mtuhumiwa huyo kudai kuwa anategemewa na familia yake na watoto wanne lakini hakimu said alisema mahakama inamuhukumu kifugo hicho, ili iwe fundisho kwa wengine kuacha ujangili

 

     Sababu za  ujangili wa Twiga

Laizer anasema  kuongezeka kwa ujangili wa Twiga kwanza kunachangiwa na kuibuka soko batili la nyama.

Anasema pia kutokana na eneo hilo kuwa a Twiga wengi, inawezekana majangili yanatumia tabia za upole wa Twiga kuwaua kirahisi  na kwa kuwa ni wakubwa wanakwwenda kuuza nyama nyingi.

“tumebaini wanauza kilo hadi sh2000 hivyo wanapata wateja wengi kulikuwa nyama ya Ng’ombe au mbuzi, sasa tunatoa elimu ambayo atakamatwa na nyama pori ataunganishwa na jangili hivyo watu waache kununua nyama hizo mitaani”alisema

Alisema wamebaini  kuna biashara hiyo, baada ya kukamata mifuko sita yenye uwezo  wa kubeba kilo kati ya 20hadi 25  ikiwa imetelekezwa baada ya kuimarishwa ulinzi.

Kamishna msaidizi mwandaizi  wa Mamlaka ya usimamizi wanyamapori(TAWA) Kanda ya Kaskazini ,Peter Banjoko anasema majangili wamekuwa wakiwindaTwiga kutokana na mbinu wanazotumia kuwakamata .

“hawa wanyama ni wakubwa hivyo, majangili wanawawinda ili kuunda nyama na vitu vingine na tutakomesha bishara  hii”anasema

Banjoko anasema kwa sasa wameimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mapito ya wanyama ili kuwadhibiti majangili.

Anasema tukio la karibunikabisa limetokea Machi 27 katika eneo la Mswakini, ambapo Twiga mmoja ameuawa, ikiwa ni takriban wiki tatu tangu kubainika kuuwa Twiga katikaeneo la Burunge WMA.

“tunashirikiana na  vyombo vingine, ikiwepo askariza burunge WMA, askari wa Chemchem  na wengine kukabiliana na ujangili huu”alisema


Asilimia ya twiga waliopotea katika kipindi cha miaka 30 iliyopita

Girrafes wamepoteza asilimia 40 ya wakazi wake katika miaka 30 tu, na ripoti za hivi karibuni zinaonyesha ujangili na usafirishaji wa wanyamapori vinachangia kupungua huku.

Meneja wa taasisi ya chem chem association, ambayo imewekeza katika eneo la Burunge  WMA, hoteli za kitalii na utalii wa picha, Walter Pallangyo alisema wameimarisha ulinzi katika eneo hilo.

“Sisi  kama taasisi ya  Mwekezaji katika eneo hili tunaamini ongezeko la shughuli za kibinaadamu katika maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za uhifadhi na Utalii ndiko kunachangia  ujangili”anasema

Anasema maeneo yamapito ya wanyama yamevamiwana kilimo ,mifugo na uvuvi na imebainika miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili wapo ambao wamekuwa wakidai kujihusisha na uvuvi ama ufugaji.

“chem chem sisi kwa mwaka tumekuwatukichangia shughuli za kupambana na ujangili zaidi yash 300 milioni”alisema.

Hata hivyo, katika uchunguzi  uliofaanywa na mwandishi wa habari hizi, kupitia mradi ya InfoNile juu ya uhalifu wa wanyamapori Afrika ya Mashariki, bado kuna tishio la  ujangili wa Twiga katika eneo hilo la ikolojia ya Tarangire na Manyara.

 

                                Kauli ya Serikali.

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro tayari alionya serikali kuwachukulia hatua  za kisheria wote ambao watabainika  kuhusika na ujangili katika eneo la ikolojia ya Tarangire na Manyara lakini pia aliagiza serikali za vijiji katika maeneo hayo kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Alisema maeneo mengi ya mapito ya wanyama yapo chini ya mamlaka za serikali za vijiji ndio sababu ni muhimu vijiji kutenga maeneo ya hifadhi, makazi na shughuli nyingine .

Hata hivyo, Katika kuhakikisha maeneo ya mapito ya wanyama yanalindwa ili kudhiti ujangili,  katika eneo laikolojia ya Tarangire na Manyara, wizara ya maliasili na Utalii tayari imeanza kuweka alama ya uambuzi wa maeneo hayo.

Afisa Maliasili ofisi ya mkuu wa mkoa Manyara,Michael Gwandu alisema katika zoezi hilo kaya zaidi ya 300 zimebainika kuishi katika maeneo ya mapito ya wanyama.

Mwandishi wa habari hizi Musa Juma akifanya mahojiano na afisa wanyama pori toka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Babati 


“kuwepo makazi na shughuli nyingine katika maeneo ya mapito ya wanyama ndio kunachangia ujangili sasa serikali imeanza tathimini ya kuona jinsi la kukabiliana na changamoto hii  na uwezekano wa kuwatafuta maeneo mbadala waliojenga katika maeneo hayo”alisema

Mkuu wa wilayaya Babati,Lazaro  Twange alisema serikali inaendelea na uchunguzi kuhakikisha wote ambao wanahusika na ujangili huu wanakamatwa.

“Tayari kuna watuhumiwa wamekamatwa na uchunguzi unaendelea kuhakikisha ujangili huu unakomeshwa, lakini pia elimu ya uhifadhi inaendelea kutolewa”alisema

Afisa wanyamapori wa wilaya Babati, Christopher Laizer pia alieleza tayari kuna mkakati wa kuhakikisha kesi zote za ujangili katika wilaya hiyo, kunakuwa na mwendesha mashitaka maalum ili kesi ziende haraka.

“wenzetu kama  shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA )wanawanasheria wao ambao wanasaidia sana hizi kesi kwenda haraka na sisi tayari tumeomba kuwa na wanasheria wetu ili kuzendesha hizi kesi kwa wakati “alisema.

Kamishna wa uhifadhi Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA), William Mwakilema alisema uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwanje ya hifadhi ni changamoto kwa sasa.

“Tunaendelea kushirikiana na vyombo vingine kuhakikisha ujangili nje ya maeneo ya hifadhi unadhibitwa kwa kushirikiana katika doria na  uchunguzi ”alisema


Habari hii uzalishaji umetokana na InfoNile na ushirikiano wa Oxpeckers Uandishi wa Habari za Uchunguzi wa Mazingira,kwa ufadhili wa Earth Journalism Network.  Vielelezo vya data–taswira na Ruth Mwizeere na Annika McGinnis / InfoNile.

No comments: