BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI NA KESI ZA UJANGILI AFRIKA MASHARIKI KUFUATILIWA NA KUDHIBITIWA KIDIGITALI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 7 July 2022

BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI NA KESI ZA UJANGILI AFRIKA MASHARIKI KUFUATILIWA NA KUDHIBITIWA KIDIGITALI











Bwana Bashiri Hangi akitoa mada ya namna ya kufuatilia biashara haramu ya wanyama pori Afrika mashariki hivi karibuni


NA: MAIPAC TEAM, Fort Portal UGANDA
 
Biashara haramu ya wanyamapori katika nchi za Afrika ya Mashiriki na kesi za ujangili zitakuwa zikifatiliwa kidijital ili kuhakikisha matukio hayo yanakomeshwa.

Mfumo wa kidigitali wa WildEye umezinduliwa  jana katika mji wa Utalii wa Fort Portal nchini Uganda na Taasisi ya InfoNile na WJA kwa kishirikiana na Taasisi ya kukusanya takwimu za wanyamapori ya Oxpeckers mradi uliodhaminiwa Shirika la misaada la kimataifa la Marekani(USAID) kupitia Internews.


Akizungumza katika uzinduzi huo, mmoja wa wakurugenzi wa InfoNile, Fredrick Mugira alisema Zana hiyo ya kidigitali itasaidia wanahabari za uchunguzi na taasisi nyingine kufuatilia na kupata takwimu za kesi na matukio ya ujangili .

"Tunatarajia wanahabari wa habari za uchunguzi wa masuala ya kufatilia ujangili na mazingira watatumia mfumo huu"alisema

Afisa wa miradi  wa Shirika la InfoNile Annika McGinnis alisema mfumo wa WildEye utawezesha wanahabari kufatilia takwimu za watuhumiwa wa ujangili tangu wanapokamatwa kesi zao hadi maamuzi ambayo yatakuwa yametolewa na mahakama.

Meneja wa mradi wa mabadiliko ya tabia wa shirika la TRAFFIC ambalo pia linajihusisha ufuatiliaji wa masuala ya wanyamapori,Jane Shuma alisema kumekuwepo na matukio ya biashara haramu ya wanyamapori na migogoro baina ya wananchi na uhifadhi.

Hata hivyo alisema katika nchi za Afrika ya Mashariki jitihada zinaendelea kuongeza uelewa  wa wananchi na ushirikishwaji wananchi katika masuala ya uhifadhi.


Akizungumzia mradi huo,Meneja wa mradi mtandao wa wanahabari masuala ya mazingira (EJN) Kiundu Waweru alisema ni faraja baada ya kupatikana wazo hilo mwaka 2020.

Waweru alisema mfumo huo umezinduliwa wakati muafaka ambapo waandishi wa habari za uchunguzi wa masuala ya mazingira na uhifadhi  24 kutoka nchi za Afrika ya mashariki Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Kenya wanashiriki katika mafunzo kuhusiana na uhifadhi na kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori.

 

No comments: