WAZIRI JANUARY MAKAMBA AITAKA BODI MPYA TPDC KUHAKIKISHA GESI NA MAFUTA YANACHANGIA UCHUMI WA TAIFA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 4 July 2022

WAZIRI JANUARY MAKAMBA AITAKA BODI MPYA TPDC KUHAKIKISHA GESI NA MAFUTA YANACHANGIA UCHUMI WA TAIFA

Waziri wa Nishati January Makamba  akizungumza na wanahabari mara baada ya kuzindua bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania  TPDC katika ukumbi wa Gran Melia Hotel jijini Arusha mapema leo 
Balozi Ombeni Sefue mwenyekiti mpya wa  Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) akizungumza na wanahabari jijini Arusha mapema leo 
Picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa kwa bodi mpya yaShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) hapa jijini Arusha

 



NA: ANDREA NGOBOLE, MAIPAC ARUSHA

Bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) imetakiwa kusaidia Taifa kufikia lengo la kuongeza mchango wa Gesi na mafuta katika uchumi wa Taifa.


Akizungumza katika uzinduzi wa bodi hiyo Leo jumatatu Julai 4,2022 jijini Arusha, Waziri wa Nishati Januari Makamba ameitaka bodi hiyo,kwenda kufanyakazi ili kutimiza ndoto ya taifa .

"Rais Samia Suluhu ana imani kubwa la bodi hii kusaidia kukuwa kiuchumi wa Gesi na mafuta hivyo tunawataka kufanya kazi vizuri zaidi "amesema 

Makamba amesema  bodi hiyo inapaswa kuhakikisha uchumi wa gesi na mafuta  unachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa taifa  na kutoa mchango kwa maendeleo na sio katika mapato bali pia katika uendelezaji wa rasilimali watu.

"Lakini pia TPDC iongeze ushiriki wa nchi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na gesi  kwa kuwa  ndio mwakilishi wa nchi"amesema

Amesema  Rais Samia Suluhu anaimani kubwa na Bodi ya TPDC kuwa itatimiza malengo ya serikali na ndio sababu alimteua, Katibu Mkuu mstaafu,Balozi Ombeni Sefuwe kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo.

"leo nimezindua bodi na tumewapa mikakati ya serikali katika uchumi wa gesi na mafuta na watakuwa hapa kwa siku mbili wakifanya semina"amesema

Naye Mwenyekiti wa bodi hiyo Balozi Ombeni Sefuwe ,amesema Bodi imejipanga kuhakikisha Taifa linakwenda kunufaika na rasilimali zake za  Gesi na mafuta .

Amesema TPDC itaendeleza mikakati ya serikali iliyopo, kutazama changamoto zilizopo na zinatatuliwa vipi ni kuhakikisha sekta ya gesi na mafuta inasaidia katika ukuaji wa uchumi.
 Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk James Mataragio ameshukuru Serikali kuteua Bodi hiyo yenye majumbe makini.

 Amesema Bodi hiyo imeteuliwa wakati muafaka ambapo TPDC inakwenda kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.













No comments: