Bilioni 889.2 zatengwa ujezi wa skimu za maji vijijini - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 20 July 2022

Bilioni 889.2 zatengwa ujezi wa skimu za maji vijijini

Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo akizungumza na wanahabari juu ya mkakati wa kujenga skimu za maji vijijini 

 .

NA: MAIPAC TEAM, DODOMA

Mhandisi Clement Kivegalo amesema  jumla ya shilingi 889.2 billion kwa ajili ya ujenzi wa skimu za maji vijijni kupitia wakala wa maji vijijini na usafi was Mazingira RUWASA kwakipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023.


“Mwaka wa fedha  2022/23 Wakala wa Maji Vjijini (RUWASA) umepanga kutekeleza jumla ya miradi 1,029 huku kati ya miradi hiyo 381 ni mipya na miradi 648 ikiwa ni ile ambayo utekelezaji wake unaendelea kutoka mwaka wa fedha uliopita,”alisema Kivegalo .

Alisema ,kukamilika kwa miradi hiyo, kutawezesha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kuongezeka kwa wastani wa asilimia sita na kwamba utekelezaji wa shughuli zake unaongozwa na Mpango Mkakati wa miaka mitano, yaani 2020/2021 hadi 2024/2025 utakaongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini hadi kufikia kiwango kisichopungua asilimia 85 kwa mwaka 2025.

Alieleza hali ya upatikanaji wa maji kabla na baada ya kuundwa RUWASA,Mhandisi Kivegalo amesema,wakati wa kuanzishwa kwake, RUWASA ilirithi jumla ya skimu za maji 1,379 zilizokuwa zimekamilika na kulikuwa na miradi 632 ya ujenzi wa skimu za usambazaji wa maji katika maeneo mbalimbali nchini na kueleza kuwa kati ya skimu hizo zilizokuwa zimekamilika 177 zilikuwa hazitoi huduma ya maji kwa wananchi kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kukauka kwa vyanzo vya maji.

Amefafanua kuwa mwezi Julai 2019 upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ulikuwa ni wastani wa asilimia 64.8 ambapo pamoja na kiwango hicho cha upatikanaji wa maji, kwa ujumla, hali ya huduma ya maji vijijini haikuwa ya kuridhisha. 
 

Sambamba na hayo katika Kijiji cha Msomera na kwamba Serikali kupitia RUWASA inaendelea na ujenzi wa bwawa la maji kwa gharama ya Shilingi bilioni 1.99 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 15

No comments: