BALOZI WA UHOLANZI NCHINI TANZANIA AFURAHISHWA NA UTENDAJI BORA WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 20 July 2022

BALOZI WA UHOLANZI NCHINI TANZANIA AFURAHISHWA NA UTENDAJI BORA WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI


Balozi wa uholanzi nchini Tanzania Balozi Wiebe De Boer akifurahia jambo na Mratibu wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa alipotembelea ofisi hizo jana

Balozi wa uholanzi nchini Tanzania Balozi Wiebe De Boer katikati alipotembelea ofisi za mtandao wa Watetetezi wa Haki za Binadamu Tanzania( THRDC)  



NA: MAIPAC TEAM

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC, unayo furaha kupata ugeni wa Balozi wa Uholanzi (Netherlands) nchini Tanzania, Balozi Wiebe De Boer.

Balozi Wiebe amefika katika ofisi za THRDC akiambatana na Afisa mkuu wa sera kutoka ubalozi huo, Wakili Chikulupi Kasaka na kufanya mazungumzo na sekretarieti ya Mtandao wa THRDC ikiongozwa na Mratibu, Wakili Onesmo Olengurumwa, pamoja na Afisa Dawati la Ulinzi la Mtandao, Wakili Paul Kisabo. 

Katika ziara hiyo balozi Wiebe amefanikiwa kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na mtandao wa THRDC katika kulinda na kutetea watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania, amejadiliana na kujifunza kwa undani kazi zinazofanywa na mtandao, ikiwa ni pamoja na kufahamu hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania na kuangalia mbinu zinazoweza kutumiwa  na Ubalozi huo kuendelea kuboresha na kuendeleza mashirikiano yake na mtandao wa THRDC.

Kwa muda sasa THRDC imekuwa na mashirikiano ya karibu na ubalozi wa Uholanzi, hii ni katika kuhakikisha watetezi wa haki za binadamu wanatengenezewa mazingira salama na rafiki katika utekelezaji wa shughuli za utetezi lakini pia wanalinda na kutetea haki za binadamu nchini.

 

 

No comments: