WASICHANA WA JAMII ZA PEMBEZONI WAFUNDWA KUJITAMBUA, KUJITHAMINI ILI KUTIMIZA NDOTO ZAO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 28 July 2022

WASICHANA WA JAMII ZA PEMBEZONI WAFUNDWA KUJITAMBUA, KUJITHAMINI ILI KUTIMIZA NDOTO ZAO

baadhi ya wanafunzi wa kike wa sekondari zilizopo wilayani Arumeru wakipatiwa mafunzo ya kujiamini, kujithamini na kujitambua ili kufikia ndoto zao kwa manufaa ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla

Baadhi ya wasichana wa shule za sekondari wakifurahi mara baada ya kupewa mafunzo ya Good Girls yaliyotolewa na taasisi ya Ndoto zetu hivi karibuni

Baadhi ya watoto wa shule za msingi wakipatiwa mafunzo ya mbinu za maisha, utambuzi na uendelezaji wa vipaji vyao katika taasisi ya Ndoto zetu jijini Arusha

 

NA: MAIPAC TEAM, ARUSHA

Jumla ya wanafunzi wa Kike 130 wa shule za sekondari wilayani Arumeru, Mkoani Arusha wamenufaika na mafunzo ya kujitambua, kujithamini na kujiamini ili kutimiza Ndoto zao. 

Mafunzo hayo yametolewa na shirika lisilo la kiserikali la Ndoto zetu lililopo jijini ARUSHA, ikiwa yamelenga kuwajengea uwezo wasichana hao kujiamini na kujitambua ili kuwa wanawake majasiri na viongozi Bora wa familia nyakati zijazo.

Akizungumza na wanahabari, Afisa miradi wa shirika Hilo, Raymond Chambo amesema kuwa wasichana hao wanasoma katika shule za sekondari Olchoki, Kiurei, Olturoto na Onyoito zote zipo wilayani Arumeru mkoani ARUSHA.

Chambo amesema kuwa waliona kuwa wasichana hao wapo katika mazingira hatari zaidi ya kupotea na kutimiza Ndoto zao pale wasipopata mafunzo sahihi ya kujitambua, kujithamini na kujiamini ili wawe chachu ya mafanikio kwa ngazi ya familia na tifa kwa ujumla.
contact infomation through +255756064900  or +255759744701

Amesema kuwa wasichana hao wameendelea kuwa mfano Bora kwa familia zao na shule zao kwani ufanisi umeongezeka katika masomo Yao, uwezo wa kutambua na kuzikabili changamoto mbalimbali za Maisha umekuwa wa manufaa makubwa kwao.

Aidha Chambo anaeleza kuwa shirika Hilo la Ndoto zetu kwa muda wa miezi 18 sasa limefanikiwa pia kutoka mafunzo kwa Kaya 13 zenye jumla ya watoto 26 kwa kuwapatia mafunzo ya kuwa na Afya Bora, kuandaa chakula Bora, maji Safi na salama na mazingira salama ya malazi, pia kuwajengea upendo kwa familia zao, Hali inayopelekea kupunguza idadi ya watoto wa mitaani na kuwa na vituo vingi vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu.

Amesema upendo ndiyo nguzo kuu ya kutengeneza familia iliyo bora kwani kukikosekana upendo ndani ya familia ndiyo hupelekea watoto kutopapenda nyumbani na kukimbilia mitaani ambapo huweza kupotea kabisa na kuua ndoto zao walizokuwa wamejiwekea maishani mwao.



No comments: