![]() |
| Wakazi wa kijiji cha Ngoswak wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa darasa la MEMKWA na shirika la CORDS |
![]() |
| Wakazi wa kijiji cha Ngoswak Kata ya Engarenaibor wakifurahia darasa hilo |
![]() |
| Akina Mama wa Kimasai waakiwa na nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa darasa hilo na kuahidi kuwaleta watoto wao waaje wasome |
![]() |
| Uongozi wa kata ya Engarenaibor na halamshauri ya longido wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa CORDS LILIAN LOOLOITAI na mdhamini wa darasa hilo ADRIAN SCOTT toka Australia |
![]() |
| Wakiwa na Nyuso za furaha ndani ya darasa la Memkwa pamoja na mfadhili wa darasa hilo Adrian Scott toka Douglas Foundation |
Mwandishi wetu, longido
Taasisi ya Utafiti,Maendeleo na Huduma kwa jamii(CORDS) imekabidhi darasa lililojengwa maalum kwa Vijana wa jamii ya Kimasai wa kike na kiume ,ambao wamekosa fursa ya kusoma katika mfumo rasmi shule ya Msingi(MEMKWA)
Darasa hilo limegharimu kiasi cha sh 33.5 milioni lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 45 na litakuwa katika shule ya msingi Ngoswak iliyopo kata ya Engareinabor wilaya ya Longido mkoani Arusha na limejengwa na shirika hilo la CORDS
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa darasa hilo, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Longido, Simon Laizer alishukuru shirika la CORDSna wafadhili shirika la Douglas Scott Foundation la nchini Australia kupitia mradi wa action on poverty. kujenga darasa hilo.
"Darasa hili litasaidia sana vijana ambao hawakusoma katika mfumo rasmi wake hapa kusoma na hivi kupambana na ujinga na umasikini"alisema
Mkurugenzi wa shirika la CORDS Lilian Looloitai alisema darasa hilo litakuwa fursa ya pekee kuwasaidia watoto husuani wa kike ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na shule kwa wakati.
Alisema kuwa mazingira ya jamii za pembezoni hususani wafugaji wa kimasai zinazokabiliwa na changamoto nyingi ambazo hupelekea watoto kutopata nafasi ya kuanza masomo kutokana na kukosekana madarasa maalum ya Memkwa ambayo huwapelekea kutokuwa na ari ya kuanza kusoma masomo hayo ya elimu ya msingi.
Amesema mwaka 2019 na 2020 walikuwa na mradi wa kuandikisha wanafunzi wa Memkwa wapatao 20 na kuanza kufundishwa shuleni hapo lakini kutokana na kukosa chumba maakum cha kuwafundishia walipelekwa shule ya msingi.
Mkurugenzi wa shirika la Douglas Scott foundation toka Australia,Adrian Scott amesema kuwa wanafurahi kusaidia ujenzi wa darasa hili kwani litasaidia kuondoa ujinga kwa watoto na pia kuwezesha kujikwamua kiuchumi
Naye mkuu wa shule hiyo Kwamboka Nyanami Phirace amewashukuru Cords kwa kuwajengea darasa hilo na kuahidi kushirikiana na uongozi wa kijiji kuhamasisha wazazi kuandikisha wanafunzi wa kutosha darasa hilo na wataanza masomo yao rasmi January 2023


.jpg)


.jpg)
No comments:
Post a Comment