![]() |
| Baadhi ya miili ya Twiga ambayo ilikutwa hivi karibuni ndani ya eneo la Jumuiya ya hifadhi ya jamii Burunge (WMA) |
NA: MAIPAC TEAM, BABATI
Taasisi ya Chem chem Association ambayo imewekeza shughuli za Utalii na uhifadhi katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya jamii ya Burunge imezindua kampeni ya Kuzuia mauwaji ya Twiga katika eneo hilo.
Burunge WMA ipo kati kati ya hifadhi za Taifa ya Tarangire na Manyara mkoa Arusha na katika miaka ya Karibuni kumekuwepo na matukio ya ujangili wa Twiga.
Wananchi kadhaa tayari walikamatwa wilayani Babati,na baadhi kufikishwa mahakamani huku mmoja akifungwa kutokana na kukutwa na nyama ya Twiga.
Akizindua kampeni hiyo, Katibu Tawala mkoa wa Manyara Carolina Mtakula katika tamasha la Chem chem 2022 katika viwanja vya Mdori wilayani Babati,mkoa Manyara, Mtakula amewataka wakazi wa vijiji ndani ya hifadhi ya jamii Burunge kushiriki katika kupiga vita Ujangili hasa wa Twiga ambao ni nembo ya Taifa.
"Tunaomba jamii ishiriki kupambana na Ujangili katika eneo hili kwani wanyamapori wanafaida kubwa kwa maendeleo ya Taifa "amesema
Awali Afisa Miradi wa Chem chem Hamis Giori amesema Taasisi hiyo imekuwa ikiandaa matamasha kila mwaka na huu ni mwaka wa nane.
Giori amesema lengo la tamasha hilo ambalo huandamana michezo mbalimbali lengo lake ni kupiga vita Ujangili, kuhifadhi Mazingira na Kuzuia ukataji wa Miti.
Msimamizi wa maeneo ya hifadhi za jamii nchini kutoka wizara ya Maliasili na Utalii Fidelis Kimario alitaka jamii kushiriki katika kupambana na majangili na kueleza wananchi wanaoishi eneo la Burunge WMA imenufaika sana na miradi wawekezaji
Kimario amesema hifadhi za jamii zinafaida kubwa kwani zipo maeneo ya mapito ya wanyama ambayo yanahitaji kutunzwa
Burunge WMA inaundwa na vijiji 10 ambavyo kila Kijiji kimetoa eneo lake kwa ajili ya shughuli za uhifadhi.


No comments:
Post a Comment