WAANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI BUNIFU ZINAZOCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI NA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 7 November 2022

WAANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI BUNIFU ZINAZOCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI NA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Mwenyekiti wa Bodi ya chuo  Cha uandishi wa HABARI Fanikiwa Ndugu Elson Makaye akizungumza na wahitimu pamoja na wazazi katika mahafali hayo

Mwanafunzi Bora Lightness Mika akipokea tuzo na cheti Toka Kwa mgeni rasmi Mussa Juma

Mussa Juma Mkurugenzi Maipac na Mjumbe wa Bodi Misa- tan akitoa nasaha Kwa wahitimu wa fani ya HABARI chuo Cha uandishi wa HABARI Fanikiwa Arusha

Mhitimu Amina Chadua akipokea cheti Cha uongozi Toka Kwa mgeni rasmi katika mahafali hayo


Mjumbe wa Bodi Fanikiwa Journalism School Arusha Elson Makaye kushoto akimkabidhi cheti Cha shukrani mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya chuo hicho

Utoaji wa tuzo Kwa wahitimu na WANAFUNZI wanafanya vizuri ukiendelea

Picha ya pamoja meza kuu na wahitimu

Baadhi ya wazazi wa wahitimu wakiwa na nyuso za furaha

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye manufaa Kwa jamii Kwa kuandika habari bunifu zinazolenga kuwakwamua wananchi  kuondokana janga la umaskini.

 Sekta ya habari na utangazaji ikitumika ipasavyo hususani vyombo vya habari mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia  vinaharakisha  zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka  zaidi hivyo kuwa chachu ya mabadiliko

 Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya wanahabari inayosaidia jamii za pembezoni nchini MAIPAC, Bw Musa Juma amesema hayo wakati akihutubia wahitimu na wazazi katika mahafali ya 16 ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Fanikiwa Arusha yaliyofanyika hivi karibuni.

 Amesema kuwa ulimwengu wa sasa umekuwa, haswa  katika eneo la sayansi na teknolojia hivyo wana habari wanapaswa kukimbia na ukuaji huo wa teknolojia kwa kuandika habari Bora na bunifu pia kuanzisha vyombo vya habari vya mitandaoni ambavyo  vitawasaidia wao kujiajiri.

Hata hivyo ameeleza kuwa  waandishi wengi wanaweza kufungua "Blog, radio mtandao na  Tv za Mitandaoni ambazo  wanaweza kupeleka maudhui mbali mbali ya kihabari na kupitia vyombo hvyo watapatikana wawekezaji mbalimbali ambao wataweka matangazo ya biashara zao ili zionekane na watazamaji au pengine wasomaji.

Musa Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi MISA - TAN na Mkuu wa magazeti ya mwananchii Mkoani Arusha amewataka wahitimu hao wa ngazi ya Stashahada kuzingatia maadili wawapo kazini lakini pia kuwa wabunifu katika kuandika habari za mazingira, kilimo, uchumi, na  mabadiliko ya TABIA NCHI ili kusaidia kuwaweka katika mazingira mazuri zaidi ya kihabari.

Naye mkuu wa chuo hicho Bwana Andrea Ngobole, amewataka wazazi  wa wahitimu    kuwaendeleza zaidi vijana hao katika chuo kikuu ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya tasnia ya habari na sekta nyinginezo.



No comments: