WATU SITA WAKIWEMO MUME NA MKE WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI KITETO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 8 November 2022

WATU SITA WAKIWEMO MUME NA MKE WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI KITETO

 WATU sita kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, sita wa kada ya afya na mmoja mwalimu, wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali maeneo ya  pori namba moja Wilayani Kiteto Mkoani Manyara.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kiteto, marehemu wawili ni mtu na mke wake, na walikuwa na mtoto wao wa miezi tisa ambaye amenusurika
Akithibitisha ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga amesema majeruhi watano wamepelekwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi na wawili wamebaki katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.
Amesema ajali hiyo ilihusisha Gari la wagonjwa wa kituo cha afya Sunya likitokea  Kibaya kupeleka Mgonjwa, ambapo baada ya kumshusha Mgonjwa njiani likagingana uso kwa uso na gari aina ya Prado ambayo ilikuwa inatokea Kilindi kuelekea Kibaya.

No comments: