JOWUTA YAPATA VIONGOZI WAPYA, SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 29 January 2023

JOWUTA YAPATA VIONGOZI WAPYA, SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO

 

Meza kuu wakiiimba wa mshikamano daima kabla ya kuanza kwa mkutano Mkuu



Mwandishi wetu,Dodoma

Chama wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania(JOWUTA) kimepata viongozi wapya ambao wataongoza chama hicho kwa miaka mitatu katika mkutano Mkuu uliofanyika hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Viongozi wapya wa chama hicho, wamechaguliwa juzi katika mkutano Mkuu wa JOWUTA ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya habari, Mhandisi Kundo Methew.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Msajili wa vyama vya wafanyakazi nchini, Pendo Perega, Afisa Kazi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Kamishna wa kazi Makao makuu Dodoma, Honesta Ngolly, Naibu Mkurugenzi Idara ya habari ya Maelezo, Rodney Thadeus na Mkurugenzi wa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) Kenneth Simbaya.

Mkutano Mkuu huo wa pili JOWUTA , ulidhaminiwa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Mamlaka ya Mwasiliano nchini (TCRA) Mfuko wa pensheni wa ( PSSSF ), Wakala wa barabara (TANROADS) Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) na Taasisi ya Wanahabari ya usaidizi wa jamii za pembezoni  MAIPAC. 

 Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo, Honesta Ngolly kutoka Ofisi ya Kamishna wa kazi Makao makuu, alimtangaza mwandishi mwandamizi wa magazeti ya Mwananchi Communication Ltd, Mussa Juma kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa JOWUTA baada ya kupata kura 58 kati ya 61 mbili zikiharibika na Moja ya hapana na alikuwa mgombea pekee.


Ngolly alimtangaza Saphia Ngalapi kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti baada ya kupata kura 42 dhidi ya Bahati Nyakiraria aliyepata kura 18, wakati Suleiman Msuya alichaguliwa tena kwa Katibu Mkuu baada ya kupata kura 42 dhidi ya Mike Mande aliyepata kura 19.


Katika Uchaguzi huo, Lucy Ngowi alishinda nafasi ya Mweka hazina kwa kupata kura 49 dhidi ya Grace Mwakangare aliyepata kura 12.


Ngolly alimtangaza Said Mmanga kushinda nafasi ya naibu Katibu Mkuu baada ya nafasi huyo wagombea kuingia katika duru ya pili ,Mmanga alipata kura 33 dhidi ya kura 26 za Robinson Wangaso ambapo awali Sangito Msafiri alipatakura 9


Katika Uchaguzi huo walichaguliwa wajumbe watatu wa bodi ya udhamini ambao ni Rutta Robert aliyepata kura 51,Tausi Mbowe aliyepata kura 43 na Claud Gwandu kura 27.


Akizungumza baada ya kuchaguliwa Juma, ambaye pia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) aliahidi kushirikiana na viongozi wengine na Serikali kudai maslahi bora kwa wanahabari.


Juma alisema kwa kuzingatia sheria JOWUTA itaungana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha waandishi wanaofanyakazi kuwa na mikataba ya kazi, kuwa na bima na kuwataka waandishi nchini kujiunga na JOWUTA.


"Lakini pia kama ambavyo alishauri Msajili wa vyama tutahakikisha ndani ya muda mfupi tunakuwa na mpango mkakati wa kazi (Strategic plan) Ili JOWUTA iweze kuwa na sehemu ya kuanzia kufanya kazi na kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato.

   

Wajumbe baraza la JOWUTA na Kamati tendaji

Mussa Juma mwenyekiti mpya wa JOWUTA akizungumza mbele ya wajumbe wa mkutano Mkuu mara baada ya kuchaguliwa

          



Katika mkutano huo, kila mkoa ulichagua mjumbe mmoja wa baraza la wafanyakazi na mjumbe mmoja kila Kanda kuunganisha kati Utendaji kazi.


Bahati Nyakiraria alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati Utendaji kutoka Kanda ya kaskazini, Ratifa Ganzel Kanda ya Mashariki na Grace Mwakalinga Kanda ya juu kusini.


Wengine ni Robinson Wangaso Kanda ya Ziwa, Mwajabu Hoza Kanda ya Magharibi, Editha Majura (Kanda ya Kati).


Waliochaguliwa baraza la wafanyakazi ni Nasra Abdalah (Dar es Salaam) Emanuel Ibrahim (Geita) Witney Joseph (Mara) Seif Mangwangi (Arusha) Rehema Cleopas (Tabora) na Msafiri Sangito (Pwani),Ashura Kazinja (Morogoro) na Asha Mwakyonde(Dodoma).


Wengine waliochaguliwa kuwa wajumbe wa baraza ni pamoja na Elizabeth Nyivambe (Mbeya), Beatha Yosam ( Njombe) na Adela Madyane ( Kigoma).


Akifungua Mkutano huo kwa niaba ya mgeni rasmi, Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya habari Maelezo, Rodney Thadeus alisema serikali itashirikiana na JOWUTA na akataka waandishi wa habari nchini kujiunga na JOWUTA Ili iwe rahisi kutatua changamoto zao.


Kwa upande wake Msajili wa vyama vya wafanyakazi Pendo Perega alipongeza JOWUTA kufanya mkutano Mkuu kwa kuzingatia sheria na taratibu na kuahidi kushirikiana na chama hicho Ili kuwasaidia wanachama wake.


Viongozi waalikwa wakishuhudiaambo mbalimbali katika mkutano Mkuu wa JOWUTA



Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya pia aliahidi UTPC kushirikiana na JOWUTA na kueleza tayari wameingiza JOWUTA katika mpango kazi wake kwa kuzingatia bila maslahi bora kwa waandishi hata uhuru wa habari haitakuwa na faida kubwa.


No comments: