![]() |
| Mbunge viti malum Mkoa wa Dodoma,Marium Ditopile akiwa na wanafunzi alupowatembelea kwa kuwapatia vifaa mbalimbali vya shule. Picha na Shakila Nyerere |
Na Shakila Nyerere, Maipac
MBUNGE viti Maalum Mkoa wa Dodoma anayetokana na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mariam Ditopile amewawezesha wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu vifaa vya shule kwa wanafuzi 1000 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 30.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma, Ditopile amesema amefanya hivyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais na pia kusherehekea kumbukizi ya Kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassani.
Aidha Amewaomba Wadau Mbalimbali Nchini Kutoa Kipaumbele Zaidi Katika Sekta ya Elimu kwa kutoa misaada hasa kwa Watoto yatima na wenye Mazingira Magumu yatakayo sababisha Kukatisha Masomo na kupoteza Ndoto zao Katika kupata elimu Bora
Naye Mwanaisha Juma Mwanafunzi wa kidato Cha tatu Katika shule ya Kwapakacha wilayani Kondoa ametoa shukrani Kwa niaba ya wenzake kwa msaada huo nakumuombea Dua Mh Marium Ditopile kwa namna alivyoguswa Katika suala Zima la kuigusa Elimu


No comments:
Post a Comment