MLIMA KILIMANJARO KUFANYA JUBILEE YA MIAKA HAMSINI MACHI 16 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 21 February 2023

MLIMA KILIMANJARO KUFANYA JUBILEE YA MIAKA HAMSINI MACHI 16





NA: MWANDISHI WETU
maipacarusha20@gmail.com


 Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro
 Machi 16 Mwaka huu inatarajia kuadhimisha jubilee ya miaka hamsini Toka kuanzishwa kwake.


Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho alisema maadhimisho hayo ya kwanza ya aina yake , yanalenga pia kuutambulisha umma kuwa mlima huo unapatikana katika nchi  ya Tanzania.




Amesema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Marangu, mkoani Kilimanjaro, huku Makamu wa Rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni Rasmi.


Alisema maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya mlima Kilimanjaro ni utaratibu wa kawaida wa Tanapa na hii ni baada ya kufanya maadhimisho kama hayo ya miaka 60 ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti.




"Kilele cha Mlima kilimanjaro kitafanyika Marangu Mkoani Kilimanjaro yalipo makao makuu ya Mlima huo huku makamu wa rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni rasmi "


Alisema mlima huo wenye urefu wa kilometa 5,895 ulianzishwa rasmi kama hifadhi ya Taifa Kilimanjaro , Machi 16, Mwaka1973 kwa ajili ya shughuli za utalii.


Naye kamishna msaidizi wa hifadhi,Angela Nyaki ,alisema  maadhimisho hayo yataanza Machi 1, hadi kilele machi 16 mwaka huu,na mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo usafi wa Mlima utakaofanyika kwa siku kumi kuanzia machi 1,ambapo wadau wa utalii wapatao 500 watashiriki.




 Shughuli zingine zitakazofanyika katika sherehe za maadhimisho hayo ni pamoja na ugawaji na upandaji wa miti, zoezi litakalozinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.


"Pia tutawatembelea waongoza utalii wa miaka ya 70 ili kuzungumza nao na kupata uzoefu wao na ushauri wao"


Alisema tangu kuanzishwa kwa shughuli za utalii katika mlima Kilimanjaro, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo ongezeko la watalii na kufikia elfu 50 kwa mwaka, kuongezeka kwa njia za kupandisha mlima huo kutoka njia moja hadi kufikia njia sita

No comments: