Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza na Kamati ya magonjwa ya mlipuko |
Kamati ya magonjwa ya mlipuko Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa |
NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA
maipacarusha20@gmail.com
MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, ameilekeza kamati ya kuelimisha jamii dhidi ya magonjwa ya Mlipuko kuweka mikakati ya kushughulikia vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na watoto wa mkoa huo.
Kunenge ametoa rai hiyo mjini Kibaha wakati akifungua kikao cha kuijengea uwezo kamati hiyo ambayo imehusisha makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, watu wenye ulemavu na wataalamu wa idara ya afya.
Amesema Mkoa huo bado una tatizo kwenye vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji kwa kundi hilo la watoto na wanawake hivyo inatakiwa kuwekewa mkazo na kamati hiyo kupinga matukio ambayo yanatokea mara kwa mara.
Kunenge ameipongeza Serikali na shirika la afya Duniani (WHO) kwa jitihada kubwa wanazozifanya za kukabiliana na magonjwa hayo hatari katika jamii hususani ya mlipuko ambayo yamekuwa kikwazo cha mipango ya maendeleo.
Ameielekeza kamati hiyo kuzingatia mfumo wa ushirikishwaji kwenye jamii ili kufanikisha malengo ya kuundwa kwa kamati hizo na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kwa kutoa elimu kwenye maeneo mbalimbali.
Kamati hizo tayari zimeundwa katika ngazi ya wilaya za mkoa huo wajumbe wakiwa ni
vongozi wa dini, watumishi idara ya afya, baadhi ya wataalamu wa Halmashauri na zitakuwa endelevu na zikijikita kwenye kutoa elimu kwenye maeneo yao ikiwemo nyumba za ibada ili jamii iwe na uelewa kuhusiana na magonjwa ya Mlipuko.
Wizara ya Afya na Shirika la Afya duniani WHO ambao ndio wafadhili wanacholenga kwasasa ni kuona jamii inakuwa na uelewa kuhusiana na magonjwa ya mlipuko kwenye maeneo yao.
Mikoa mingine ambayo imeunda kamati kama hizo ni Tanga, Pwani, Geiita na Manyara na imeelezwa kuwa endapo mikoa hiyo itafanya vizuri mikoa mingine itafikiwa kwa kuanza kuunda kamati kama hizo
No comments:
Post a Comment