Mwanafunzi akutwa amejinyonga Chumbani kwake Kibaha - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 20 February 2023

Mwanafunzi akutwa amejinyonga Chumbani kwake Kibaha

 


NA:JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA



MWANAFUNZI wa darasa la nne (10) Tatu John shule ya Msingi Kambarage Halmashauri ya Mji wa Kibaha amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba kwenye chumba cha kulala nyumbani kwao Kibaha

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mkoani B Shabani Rashid alisema alipokea simu kutoka kwa mjumbe wa mtaa wake  akimueleza kuwa kuna mtoto amejinyonga ndani ya nyumba.

Rashid amesema majira ya saa tisa kasoro alasiri Februari 19 alipigiwa simu na mjumbe huyo na kabla hajaenda alitoa taarifa polisi ili wafike kwenye eneo la tukio.

Amesema alipofika alikuta wafiwa wapo na mjumbe, ndipo walipoingia ndani ulipo mwili wa marehemu na kuukuta akiwa  ameingiza kichwa ndani ya kamba ya neti ambayo imefungwa dirishani mkono wa kulia na kushoto.

" Eneo la tukio ni dirishani kwenye chumba ambacho walikuwa wanalala watoto, na tulimkuta marehemu amepiga magoti, polisi walifika wakapiga picha na kuchukua alama zao kisha wakaondoka na mwili kuupeleka Tumbi Hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi" amesema.

Amesema Wananchi wanaoishi mkoani B wamepata taharuki kwa mtoto wa miaka kumi daarasa la nne kuchukua maamuzi ya kujinyonga

Amewashauri wazazi kujenga ukaribu na watoto wao pamoja na kuuimarishe ulinzi katika familia hasa kwa watoto ili kujua vikwazo wanavyokutana navyo na kuvitatua kabla havijaleta madhara.

Baadhi ya majirani ambao hawakutaka kutaja majina yake wamesema tukio hilo limegubikwa na utata kutokana na mazingira yake ambapo inadaiwa marehemu alikutwa amepiga magoti baada ya kujinyonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema uchunguzi unaendelea.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi ukisubiri taratibu za mazishi

No comments: