Mbunge wa Jimbo la Monduli,Fred Lowassa Akizungumza na wakazi wa Kata ya Naalarami jioni ya leo |
Mwandishi wetu, Maipac Monduli
maipacarusha20@gmail.com
Serikali yaridhishwa na mikakati ya wilaya ya Monduli, mkoani Arusha kuboresha sekta ya Mifugo kutokana na ujenzi wa miundombinu na kuboresha Minada
Naibu Waziri wa maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega ametoa pongezi hizo Leo February 20,2023 wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Naalarami na viongozi wa Serikali wilayani Monduli.
Waziri Ulega amesema miundombinu ambayo imeendelea kuboreshwa na wilaya ya Monduli itasaidia sana kukuwa kwa sekta ya Mifugo.
Naibu Waziri Ulega amewataka wafugaji katika wilaya hiyo kuanza kufuga kisasa ikiwepo kutenga maeneo ya nyanda za malisho ili kukabiliana na Ukame.
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fred Lowassa Akizungumza katika ziara hiyo, amemshukuru Naibu Waziri wa Mifugo, Ulega kutembelea jimbo la Monduli kukagua miundombinu ya mifugo .
Lowassa amesema Wananchi wa Kata ya NAALARAMI wamefarijika sana kwa ugeni huu na wametuma salamu za Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia sekta ya Mifugo.
Amesema katika wilaya hiyo ,ambayo ni ya wafugaji wanamkakati wa kuwasaidia wafugaji kielimu Ili iwe rahisi kuboresha maisha yao badala ya kuwasisitiza wauze mifugo.
"Hawa ndugu zangu kazi ambayo wanajua ni ufugaji pekee hawajuwi biashara nyingine zaidi ya mifugo Sasa mikakati yetu ni kusomesha vijana wengi zaidi Ili kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuamini vijana watakuja na ujuzi tofauti"amesema
Lowassa amesema Rais Samia amesikia kilimo Chao Cha maji , barabara na soko la akina mama wa mji wa mto wa mbu .
"Tunashukuru sana Rais Samia amekubali maombi yangu na barabara ya kilomita 20 kutoka Kigongoni hadi Engaruka inajengwa lakini pia analeta mradi wa maji na anajenga soko la wanawake Mtowambu "amesema
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Selemani Mwenda akizungumza na wakazi wa Kata ya Naalarami wilayani MONDULI huku Naibu Waziri wa wa maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akimsikiliza kwa makini |
Mkuu wa wilaya ya Monduli Selemani Mwenda amesema wilaya hiyo imejipanga vyema kutatua kero za Wananchi wa Monduli na kuna Mahusiano mazuri baina ya Mbunge na watendaji wa Serikali.
No comments:
Post a Comment