RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI, AMTENGUA WAZIRI WA MIFUGO, AMTEUA MWANAFA KUWA NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 26 February 2023

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI, AMTENGUA WAZIRI WA MIFUGO, AMTEUA MWANAFA KUWA NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO

 NA: ANDREA NGOBOLE, MAIPAC

 maipacarusha20@gmail.com

Rais Dkt. Samia Suluh Hassan amefanya uteuzi wa Waziri, NaibuWaziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu wakuu pia kuwahamisha wizara baadhi ya Manaibu mawaziri na kuwatengua baadhi ya mawaziri na Mkuu wa mkoa.

kwa mujibu wa taarifa ya IKULU iliyotolewa leo jumapili na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt.Mosses M. Kusiluka imesema kuwa Mheshimiwa Abdallah Hamis Ulega ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na kuchukua nafasi ya Mashimba Ndaki ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya hapo Mheshimiwa Ulega alikuwa naibu Waziri katika Wizara hiyo ya Mifugo na Uvuvi.

https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2020/11/HAMIS2.jpg
Mheshimiwa Hamisi Mohamed Mwinjuma akila kiapo cha utiifu Bungeni jijini Dodoma ambaye leo ameteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluh Hassan  kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo


Taarifa imesema kuwa Mheshimiwa Hamisi Mohamed Mwinjuma ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchukua nafasi ya Pauline Gekul ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

kwa taarifa zaidi za wateule wengine soma hapa chini katika taarifa rasmi ya IKULU.

No comments: