Dkt Tulia Ackson aongoza kikao cha Kundi la SADC - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 10 March 2023

Dkt Tulia Ackson aongoza kikao cha Kundi la SADC

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungato Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao Cha kundi la SADC





Spika wa Bunge Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo Machi 10, 2023 ameongoza Kikao cha Kundi la SADC katika Umoja wa Mabunge Duniani (SADC Geopolitical Group in the IPU) kilichofanyika katika Ukumbi wa Paddock 6, Bahrain International Circuit (BIC), Manama, Bahrain kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Katika mkutano huo, Mhe. Spika ameambatana na Wabunge Wawakilishi wa Bunge la Tanzania kwenye Umoja huo ambao ni Mhe. Dkt. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu, Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ulenge, Mhe. Ramadhan Ramadhan, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa J. Mwihambi, ndc.....

No comments: