WAZIRI MKUU AHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UCHUMI WA MWANAMKE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 10 March 2023

WAZIRI MKUU AHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UCHUMI WA MWANAMKE


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Mwanamke Kiongozi kwa mwaka 2023




NA: Mwandishi Wetu
maipacarusha20@gmail.com

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanawake wote na Watanzania kwa ujumla waendelee kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotokana na matumizi ya teknolojia katika kujenga uchumi wa kidijitali.

Ametoa wito huo leo wakati akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Mwanamke Kiongozi kwa mwaka 2023 uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo uliambatana na mahafali ya nane ya Programu ya Mwanamke Kiongozi ambapo jumla ya wahitimu 65 walitunukiwa vyeti. Washiriki 11 wa Programu hiyo walijidhamini wenyewe na wengine 54 wanatoka kwenye kampuni 29.

Akitoa msisitizo kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo, Waziri Mkuu amesema: “Wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki katika programu hii kwani imeendelea kuwa na matokeo chanya kwa washiriki na kuleta mabadiliko makubwa kwenye utendaji wao wa kazi na kugusa maisha yao binafsi.

“Nitoe rai kwa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kiendelee kutoa mafunzo haya ya uongozi kwa wanawake pamoja na kuendelea kuwa vinara katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa maeneo ya kazi.”amesisitiza Kassim Majaliwa, waziri mkuu

Ameongeza kuwa suala la mabadiliko ya kidigitali ni moja ya vipaumbele vya Taifa kwani maendeleo ya uchumi yanategemea sana utandawazi.

“Lakini pia katika mabadiliko haya ni muhimu kutambua mchango wa wanawake katika uchumi wetu na kutatua changamoto zinazowakabili wanawake ili waweze kushiriki kikamilifu katika masuala ya uchumi wa kidijitali.” Amesisitiza Waziri Mkuu

No comments: