GODBLESS LEMA ATAJA SABABU ZA KUTOKUJA NA FAMILIA YAKE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 2 March 2023

GODBLESS LEMA ATAJA SABABU ZA KUTOKUJA NA FAMILIA YAKE

Godbless Lema akiwzungumza na wakazi waliojitokeza kumlaki

 

Na: Mwandishi Wetu, Arusha

maipacarusha20@gmail.com


Amesema kukimbia na watoto na mke ni jambo gumu lakini yeye akisikia anatafutwa inakua ni rahisi kudhibiti tatizo hilo na kwamba kama familia wamekubaliana kurudi kwa awamu pale mambo yatakapokuwa yamekaa sawa.

"Tumekubaliana turudi kwa awamu na mimi ndo nitangulie kuja kuweka mazingira mazuri, kuna vitu vingi vya kufanya na tulivyofika Canada mke wangu alianza shule na watoto pia, yule mkubwa anatarajia kuanza chuo kati ya mwezi wa saba au wa nane” amesema Lema

Lema amerejea nchini jana akitokea Canada alikokimbilia baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, alipokelewa na wafuasi na wanachadema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).


 

No comments: