Kamati ya Bunge kutembelea miradi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 14 March 2023

Kamati ya Bunge kutembelea miradi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo


Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dodoma

 maipacarusha20@gmail.com


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ipo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyotengewa fedha kwa mwaka wa 2022/2023.

 

Kamati hiyo yenye wajumbe 21 imepokea taarifa hiyo Machi 14, 2023 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akisaidiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Husna Sekikobo.

 

Miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo ni pamoja na Mradi wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambao unasimamiwa na Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambao umetengewa kiasi Shilingi 515,000,000 kukarabati kituo hicho na kuweka alama katika maeneo ya Urithi wa Ukombozi nchini pamoja na Miradi ya Maendeleo wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambayo imetengewa kiasi cha Shilingi 550,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa chuo hicho.

 

“Tumepokea taarifa yenu hapa na wajumbe tumeiona, tuna ziara ya kuja huko site kutembelea kujionea kazi iliyofanyika kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali” Mhe. Prof. Mkumbo.

 

Kamati hiyo itatembelea Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichopo Dar es Salaam Machi 18, 2023 na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Machi 18, 2023 iliyopo wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.

 

Timu ya Wizara imeongozwa na Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma, Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa, Wakurugenzi pamoja na wakuu wa taasisi ambazo zimewasilisha taarifa zao.




 

No comments: