Na Mwandishi wetu MPANDA,KATAVI
maipacarusha20@gmail.com
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewasili mkoani Katavi leo tarehe 23 Machi 2023 kwa ziara ya siku mbili mkoani humo.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Pinda atakutana na watumishi wa sekta ya ardhi wa mkoa wa Katavi, mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya pamoja na kukutana na watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ili kupokea taarifa za utendaji kazi pamoja na kutoa maelekezo.
Aidha, Mhe. Pinda atazindua Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Mlele pamoja na kukagua ujenzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) za wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Mkoa wa Katavi ni wa tatu kutembelewa na Naibu Waziri Pinda tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 26 Februari 2023 kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitokea Wizara ya Katiba na Sheria.
Mara tu baada ya kuteuliwa kutumikia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maeneleo ya Makazi Naibu Waziri Pinda amefanya ziara Mkoani Arusha na Dar es salaam ambapo amekutana na Watumishi wa Sekta ya Ardhi ili kupokea taarifa za utendaji kazi pamoja na kutoa maelekezo ya Serikali.
No comments:
Post a Comment