RIDHIWANI KIKWETE AWASIHI WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA KUEPUKA TAMAA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 19 March 2023

RIDHIWANI KIKWETE AWASIHI WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA KUEPUKA TAMAA


Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na walimu pamoja na wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kikaro

Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akikata utepe shule ya sekondari kikaro


 Na JULIETH MKRERI,MAIPAC CHALINZE


maipacarusha20@gmail.com 

MBUNGE wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amewataka wanafunzi wanaomaliza kudato Cha SITA kuepuka tamaa za Dunia na kujali masomo Yao kwanza.

ameyasema hayo aliposhiriki sherehe za kuwaaga wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Kikaro Kata ya  Miono wilayani Chalinze.

Katika sherehe hizo Mbunge huyo amewaasa wanafunzi hao kuepuka tamaa za dunia na kujali masomo kwanza kwa kuendelea na Elimu ya juu ili watimize malengo Yao.

 Katika hatua nyingine Ridhiwani ameshiriki sherehe ya Miaka 10 ya Taasisi ya Ifm Charity kwa kufungua Vyoo vilivyojengwa na Taasisi hiyo katika kituo cha kulelea watoto Yatima cha Hope- Miono.

No comments: