WAKUU WA WILAYA MNADHAMANA KUBWA KULINDA KIZAZI CHA KITANZANIA- WAZIRI DKT. GWAJIMA. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 19 March 2023

WAKUU WA WILAYA MNADHAMANA KUBWA KULINDA KIZAZI CHA KITANZANIA- WAZIRI DKT. GWAJIMA.

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima



Na WMJJWM, DODOMA

maipacarusha20@gmail.com


Rai Imetolewa  kwa Wakuu wa Wilaya nchini kuwa mstari wa mbele kubaini na kuibua mienendo isiyofaa ndani ya jamii ikiwemo vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa Mila na Desturi zilizo nje na Utamaduni wa Mtanzania.


Akitoa mada kwa Wakuu wa Wilaya Machi 17, 2023 jijini Dodoma, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Viongozi hao ni nguzo muhimu katika Mapambano dhidi ya maovu ndani ya Jamii


Amewahimiza kuwatumia Maafisa Maendeleo na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanapata taarifa sahihi kwani watumishi wa Kada hiyo wapo karibu zaidi na jamii


"Utekelezaji wa Wizara hii una mchango mkubwa katika kutengeneza watu na Taifa hili kuanzia utoto wao hivyo mkiielewa Wizara hii na malengo yake na kuelezea vizuri kwa Jamii mtaongoza vizuri" amesema Dkt. Gwajima.



Mhe. Dkt. Gwajima amewasisitiza pia kuhakikisha NGOs zinazofanya kazi kwenye maeneo yao zinafuata mikataba, kanuni na sheria ikiwemo misingi ya maadili.


No comments: