Na Mwandishi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Jeshi la Uhifadhi (JU) Hifadhi ya Taifa Ruaha kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mbeya tarehe 25.3.2023 limefanikiwa kukamata watuhumiwa watatu wakiwa na meno ya tembo.
Watuhumiwa hao Oden Mwaseba (50), Mussa Jackson (42) na Emmanuel Joseph (32) walikamatwa katika maeneo ya Uyole mkoani humo wakiwa na vipande 25 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya $120,000 sawa na Tshs 278,696,400.
Taarifa ya tukio hilo imetolewa leo jijini Mbeya, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kusaga pamoja na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi-Godwell Ole Meing’ataki ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha.
Ukamataji huo umetokana na ushirikiano baina ya Jeshi la Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa Ruaha na wananchi wanaozunguka maeneo ya Hifadhi kutokana na mahusiano mazuri ambayo yamejengeka kati yao.
Watuhumiwa wanashikiliwa katika Kituo kikuu cha Polisi Mkoani Mbeya kwa hatua zaidi za kisheria.
No comments:
Post a Comment