UWINDAJI WA KITALII WATOA BILLION 9 KWA HALMASHAURI NA VIJIJI PEMBEZONI MWA MAPORI YA AKIBA NCHINI TANZANIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 10 May 2023

UWINDAJI WA KITALII WATOA BILLION 9 KWA HALMASHAURI NA VIJIJI PEMBEZONI MWA MAPORI YA AKIBA NCHINI TANZANIA

 




Na: Mwandishi wetu

maipacarusha20@gmail.com

Uwindaji wa Kitalii Wanufaisha Nchi, Billioni 9.6 zatolewa Kwa Halmashauri na Vijiji Pembezoni mwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu - Kamishna Mabula


Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi Nyanda amesema shughuli za Uwindaji wa Kitalii zinazofanywa katika Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu  yanayosimamiwa na TAWA Nchini, zina manufaa na  mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Nchi na mwananchi mmoja mmoja hususan wale waishio pembezoni mwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu.


Ameyasema hayo leo Mei 10, 2023 katika Ofisi za Pori la Akiba Kizigo lililopo Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida akiongea na Watumishi wa Pori hilo katika ziara yake ya kikazi Kanda ya Kati.


Kamishna Mabula amesema Serikali kupitia TAWA  Tshs. Billioni 9.6 Kwa Halmashauri na Vijiji wanufaika wanaoishi pembezoni mwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu Nchini ikiwa ni fedha zitokanazo na asilimia 25 ya ada ya Wanyamapori waliowindwa pamoja na Utalii wa picha katika kipindi cha kuanzia Aprili 2022 Mpaka Desemba 2022.


Katika ziara hiyo, Kamishna Mabula amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo (ujenzi wa visima vya maji safi, nyumba za watumishi na ofisi) na  amekutana na kuzungumza na viongozi wa Kanda ya kati ya TAWA na Watumishi wa Pori la Akiba Kizigo akiupongeza uongozi wa Pori hilo na Kanda Kwa ujumla Kwa kazi nzuri wanayoifanya huku akiwahimiza kuongeza ubunifu, bidii ya kazi Ili kuongeza mapato ya TAWA na hivyo kuchangia katika pato la Taifa.


"Kwa kipindi cha Mwaka huu wa fedha tuhakikishe tunafanya kazi Kwa kujituma, Kwa bidii Ili kurudisha shukrani Kwa Serikali Kwa namna inavyotujali" amesema Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda


Kamishna Mabula amewaagiza viongozi na Watumishi wa Kanda ya kati kuhakikisha Vitalu vyote vya Uwindaji wa Kitalii katika Pori la Akiba Kizigo vinapata wawekezaji. Ikizingatiwa kuwa Pori hilo lina jumla ya Vitalu vinne vya Uwindaji ambapo viwili kati ya vinne vimepata wawekezaji


Kuhusu Wanyamapori Wakali na Waharibifu, Kamishna Mabula amesema mkazo wa Wizara na Taasisi (TAWA) ni kuhakikisha kuwa adha wanayoipata wananchi kutokana na Wanyamapori Wakali na Waharibifu inadhibitiwa kikamilifu 


"Hili suala la Wanyamapori Wakali na Waharibifu ni la kupambana nalo usiku na mchana, tupambane Kwa nguvu zote na tufanye Kila linalowezekana kuhakikisha linadhibitiwa" amesema 


Pamoja na hilo, Kamishna Mabula amesisitiza suala la viongozi wa vijiji, kata na wilaya kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria ya matumizi bora ya ardhi kwani wao ndio huwapatia wananchi vibali vya ujenzi na makazi ambapo Kwa kutoelewa wananchi huanzisha kilimo na makazi  holela na hivyo kuvamiwa na Wanyama Tembo.


Pia, ameelekeza watumishi wa Pori hilo  kuimarisha mashirikiano na Wadau wa Uhifadhi (Wildlife Conservation Society)  Ili kujenga  mahusiano mazuri na kufanya kazi Kwa kushirikiana na Wananchi Wote wanaozunguka hifadhi hiyo, Kwa kufanya hivyo watajenga taswira nzuri ya Taasisi Kwa Umma.


Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi, Kamanda wa Uhifadhi wa Pori la Akiba Kizigo Ogossy Gasaya amesema Katika kipindi Cha Mwaka 2022/2023 Pori hilo limekusanya jumla ya Tshs . Millioni Saba na Nne (704,000,000) kutokana na shughuli za Uwindaji wa Kitalii Kwa  watalii watano (5) na "observers 14 waliotembelea Pori hilo na kuahidi ongezeko kubwa la mapato  Kwa Mwaka ujao wa fedha.


Kuhusu miradi ya maendeleo Kamanda Gesaya katika kipindi cha Mwaka 2020/2022 mpaka 2023 Pori limesimamia jumla ya miradi mitano (5) ambapo minne imeisha Kwa asilimia 100 na mmoja uko asilimia 90.


Gesaya amesema baada ya kupatiwa vitendea kazi vya kutosha, hali ya ujangili imepungua Kwa kiasi kikubwa Mwaka 2022/23 ikilinganishwa na ilivyokuwa Mwaka 2021, pia mashirikiano kati ya Pori hilo, wawekezaji na Wadau wa Uhifadhi (WCS) umeboreka.


Kwa niaba ya watumishi wa Pori la Akiba Kizigo, Kamanda Gesaya ameipongeza Menejimenti ya TAWA Kwa kuboresha maisha ya watumishi kimaslahi na kuwapatia vitendea kazi jambo ambalo limeongeza morali ya kujituma katika kazi

No comments:

Post a Comment