BABA JELA MIAKA 40 KWA KUMPA MIMBA BINTI YAKE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 10 May 2023

BABA JELA MIAKA 40 KWA KUMPA MIMBA BINTI YAKE



 NA: JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA



MAHAKAMA  ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemuhukumu Fadhili Hai,(58), Mkazi wa Kwa Mfipa - Kibaha kifungo cha miaka 40 jela, viboko 12 na kulipa fidia ya sh. Milion 4 baada ya kupatikana na hatia ya kuzini na binti yake na kumsababishia ujauzito.

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 11/ 2023 imetolewa Mei 8, 2023 na Hakimu Mfawidhi Judith Lyimo wa mahakama ya Wilaya ya Kibaha wakati kesi ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Akisoma hukumu hiyo Judith Lyimo alieleza kuwa mtuhumiwa alitiwa  hatiani kwa Mujibu wa kifungu namba 158 (1) (b) na 2 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Ilielezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe Juni  05,2021 majira ya saa 09:00 alasiri huko Kwa mfipa, Wilaya ya Kibaha,Mkoa wa Pwani.


No comments: