![]() |
RAIS SAMIA SULUHU HASSANI akizungumza na wakazi wa Arusha katika siku ya kilele Cha kupinga madawa ya kulevya Nchini |
.Serikali yatangaza mkakati wa Kudhibiti biashara na Kilimo Cha bangi
Mwandishi wetu, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu bunge sera na uratibu Jenista Mhagama amesema katika mwaka wa fedha Rais Samia Suluhu Hassan ametenga shs 24.4 bilioni sawa na asilimia 100 kwa lengo la kuwasaidia vijana waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya nchini .
Ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya kupiga Vita Dawa za kulevya madawa
Amesema ,pamoja na biashara ya dawa za kulevya lengo kubwa ni kuhakikisha vijana wanakuwa salama na kuokolewa kutoka kwenye uraibu wa matumizi wa dawa za kulevya.
Mhagama amesema asilimia kubwa ya vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa katika kuleta maendeleo ndio maana serikali imeamua kuwekeza nguvu kubwa katika kuwasaidia vijana kuweza kujikwamua katika changamoto hiyo.
"serikali inatumia gharama kubwa kutibu watumiaji wa madawa ya kulevya na tayari mikakati ya kujenga kituo kikubwa cha madawa."amesema.
Kwa upande wake Kamishna wa kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya nchini Kamishna Jenerali Aretas Lyimo amesema mpaka sasa wananchi 16 wamechukuliwa hatua kwa kujihusisha na ulimaji wa zao la bangi mkoani Arusha.
Lyimo amesema elimu zaidi inaendelea kutolewa kwa wananchi katika kutambua madhara ya matumizi ya madawa hayo kwani yamekuwa yakiathiri afya za binadamu.
"Tumekuwa tukitoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya dawa za kulevya kwani zimekuwa zikileta athari kubwa kwenye ubongo wa binadamu na tunataka kuhakikisha zao hilo linaisha kabisa kwa jiji la Arusha na kwa watakaokaidi watachukuliwa hatua kali za kisheria "amesema .
Aidha ametoa wito kwa vijana waliotoka kwenye uraibu wa matumizi ya madawa ya kulevya na kuacha biashara ya madawa wana haki ya kuomba fedha katika mfuko wa halmashauri ili waweze kujiajiri pamoja na kuitaka jamii kuacha kuwanyanyapaa vijana wanaotumia madawa ya kulevya.
Kwa upande wa vijana waliotumia madawa ya kulevya wameiomba serikali pamoja na wadau kuweza kuboreshewa huduma kwa watumiaji wa madawa ya kulevya huku wakisema wamekuwa waelimisha Rika kwa jamii na kuwa mabalozi kwa jamii.
No comments:
Post a Comment