NA: Mwandishi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Ongezeko la Matumizi ya Shisha nchini, limetajwa kuchochea matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na kuvuta Shisha katika maeneo mbalimbali ya Burudani na starehe nchini.
Akizungumzia katika maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga Vita Dawa za kulevya Duniani Leo June 25,2023, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema uvutaji wa Shisha umekuwa ukichanganywa na dawa za kulevya.
Lyimo amesema ,wamebaini baadhi ya wauzaji wa Shisha kuchanganya dawa za kulevya hatua ambayo imeongeza matumizi ya dawa za kulevya nchini.
"Matumizi ya Shisha yameongeza matumizi ya dawa za kulevya na kuchochea matumizi ya dawa hizo"amesema
Hata hivyo Kamishna Lyimo hakueleza hatua zaidi kuhusiana na uvutaji wa Shisha nchini.
Hata hivyo amesema, Mamlaka hiyo imejipanga Kupambana na dawa kulevya nchini hatua ambayo imefanya Tanzania Kuwa mfano wa Kudhibiti dawa hizo .
Amesema hata hivyo umefika wakati elimu juu ya athari za dawa za kulevya kutolewa kuanzia mashuleni ili Kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na biashara hiyo
Amesema Mamlaka hiyo inakusudia kujenga ofisi za Mamlaka hiyo katika mikoa kadhaa nchini ili kuimarisha Vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Matumizi ya Shisha yaliwahi kuibua mjadala kutokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam,Poul Makonda kuipinga marufuku.
No comments:
Post a Comment