KAMISHNA WA TAWA ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA BLM PORI LA AKIBA MKUNGUNERO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 22 June 2023

KAMISHNA WA TAWA ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA BLM PORI LA AKIBA MKUNGUNERO

 




Na Mwandishi wetu, DODOMA. 


maipacarusha20@gmail.com


Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi Nyanda ameeleza kuridhishwa kwake na Kasi ya utekelezaji wa maagizo ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika Pori la Akiba Mkungunero  dhidi ya vijiji vya Kimotorok  wilayani Simanjiro na Irkiurshbor wilayani Kiteto .


Ameyasema hayo leo Juni 22, 2023 akiwa katika ziara yake ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa maagizo ya Baraza la Mawaziri ndani ya Pori la Akiba Mkungunero katika eneo linalopakana na Mkoa wa Manyara ambapo aliambatana na KU ya Mkoa wa Manyara ambayo iliwakilishwa na RPC na RSO


"Mimi kama kiongozi Mkuu wa TAWA nimeambatana na KU ya Mkoa ambayo imewakilishwa na RPC na RSO, tumefika hapa kwaajili ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa maelekezo hayo Ili kuona kama yanakwenda Kwa Kasi inayotakiwa na yatakamilika Kwa muda unaotakiwa" amesema


"..tumefika hapa tumezunguka tumejionea kinachoendelea Kimsingi tumeridhishwa na kazi inayoendelea hapa" ameongeza Kamishna Mabula


Kamishna Mabula amesema Kati ya vigingi 76 vinavyopaswa kuwekwa kama alama za mipaka ya Pori, 41 tayari vimekwishawekwa na zoezi la kukamilisha kuweka vingine 35 vilivyosalia linatarajiwa kukamilika ndani ya siku 3 kuanzia leo.


Sambamba na hilo, Kamishna Mabula amesema Serikali imemega eneo lenye ukubwa wa takribani heka 12, 644 sawa na Kilometa za Mraba 51 kutoka ndani ya Pori hilo na kuziacha Kwa wananchi.


Kufuatia ufumbuzi wa mgogoro huo uliodumu takribani miaka 20, Kamishna Mabula amesema Serikali inategemea kupata wawekezaji katika Pori hilo ambao watapelekea ongezeko la mapato ambayo yataiwezesha kuimarisha uhifadhi.


Faida nyingine za ufumbuzi wa mgogoro huo zimetajwa kuwa ni  pamoja na mipaka ya Pori kuwa dhahiri na hivyo kuwawezesha wananchi kuiona Wakati wa kutekeleza shughuli  za Kila siku na kufanya kazi zao bila bugudha na mkanganyiko na hivyo kuleta mtengamano.


Aidha Kamishna Mabula ametoa rai Kwa wananchi kuacha yaliyopita na kuongeza ushirikiano Kwa Wahifadhi katika kuhakikisha rasilimali za Taifa hili zinalindwa Kwa nguvu ya pamoja kwani wahifadhi wamepewa dhamana ya kulinda rasilimali za Nchi hii Kwa niaba yao.

No comments: