KUNENGE APONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA KIBAHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 23 June 2023

KUNENGE APONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA KIBAHA

 




NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA


MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kuongoza kimapato kwa mwaka 2022/2023.

Kunenge ametoa pongezi hizo June 22,2023 katika kikao cha baraza maalum la kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

"Upande wa asilimia mliongoza sio jambo dogo kwa Halmashauri ya Wilaya kuongoza nchi nzima, mnastahili pongezi kwa juhudi mlizoonyesha " amesema Kunenge.

Aidha Kunenge amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Butamo Ndalahwa kwa kuendelea kuaminiwa na Rais kuwatumikia wakazi Kibaha kwani utendaji na juhudi zake za kuwatumikia wanakibaha zinaonekana.

"Nanatambua kuna malimbikizo ya madeni ya wastaafu lakini Halmashauri imefanya jitihada za kulipa malimbikizo hayo na juhudi zinaendelea za kulipa madeni hayo Kadri fedha zinavyopatikana" amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata Hati Safi na kuwataka wakuu wa idara kuhakikisha hawazalishi hoja .

Nickson amewataka madiwani kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo katika kata zao ili kuepuka kuzalisha hoja za ukaguzi.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Nsajigwa George amewataka watendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanajibu hoja za mkaguzi wa ndani ipasavyo kwani hoja za CAG asilimia kubwa zinatokana na hoja za mkaguzi wa ndani.

No comments: