RAIS SAMIA SULUHU HASSANI MGENI RASMI SIKU YA KIMATAIFA KUPINGA MADAWA YA KULEVYA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 21 June 2023

RAIS SAMIA SULUHU HASSANI MGENI RASMI SIKU YA KIMATAIFA KUPINGA MADAWA YA KULEVYA

  

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza na Waandishi wa Habari 

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha 

Baadhi ya viongozi wa dini na Mila wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela 



Na Mwandishi wetu ARUSHA 


maipacarusha20@gmail.com


Rais  Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya  kupiga Vita  dawa za kulevya Dunia yatakayofanyika kitaifa Jijini Arusha june 25 mwaka huu.


Maadhimisho haya yatatanguliwa na maonesho katika uwanja wa sheikh Amri Abeid ambayo yataanza June 23 mwaka huu.



Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella akizungumza  na waandishi wa habari Leo June 21,2023 amesema maadhinisho hayo yanalengo la kupambana na kupiga vita madawa ya kulevya hapa nchini.



Mongela amesema kuwa dawa za kulevya zinaleta athari kubwa kwa jamii na zina takiwa kupingwa kwa nguvu zote ili kunusuru vizazi vijavyo kwa maendeleo ya taifa la Tanzania ili kuwa na nguvu kazi za kulijenga taifa kiuchumi.


"Maadhimisho haya kauli mbiu yake ni "Zingatia utu, kuimarisha Huduma za Kinga na Tiba", Lengo lake kubwa ni kuhakikisha kila jamii ipige vita dawa za kulevya wakiwemo viongozi wa dini na jamii kwa ujumla"amesema.


Mongela amewataka viongozi wote mkoa Arusha kushiriki katika  kudhibiti janga la matumizi ya dawa za kulevya na kuchukua hatua dhidi ya dawa za kulevya kwani kunabaadhi ya waathirika hupelekea kuwa wahalifu katika Jamii "amesema


Mongela amewaomba  wakazi wa Arusha na mikoa jirani kujitokeza katika maadhimisho hayo katika uwanja wa sheikh Amri Abeid ambapo Rais anatarajiwa kuhudhuria.


Kwa upande wao viongozi wa dini na mila Mkoa wa Arusha wameeleza kuwa jambo la kupambana na madawa ya kulevya ni jukukumu la kila mtu moja moja na siyo la serikali peke yake na viongozi wa dini.


Kiongozi mkuu wa Mila ya Kimasai,Laigwanani  Olekisongo Meijo amesema kuwa kwa wale wote wanao husika na uuzwaji wa madawa ya kulevya wachukuliwe hatua kali ili kuwa fundisho wa wengine ambao wanafanya biashara hiyo ambayo inasababisha vijana kuww tegemezi kwa familia na taifa.

Amesema viongozi wa dini na Mila wanaunga mkono jitihada za serikali Kupambana na Dawa za kulevya nchini.



No comments: